Rais wa Kenya William Ruto ameamua kuutema muswada wa fedha 2024 / picha:Ikulu Kenya 

Maandamano nchini Kenya yaliyoongozwa na vijana yamepinga kuidhinishwa kwa muswada wa fedha 2024. Rais wa nchi hiyo William Ruto ameamua kuutema muswada huo akidai amesikiliza sauti za wananchi.

Ibara ya 115 ya Katiba inampa Rais mamlaka ya kurudisha Muswada Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa upya, ikibainisha mashaka yoyote ambayo Rais anaweza kuwa nayo kuhusu Mswada huo. Baada ya hapo, Bunge linatakiwa kuzingatia kutoridhishwa kwa namna iliyoainishwa chini ya Ibara ya 115 ya Katiba.

Waraka wa Rais umerudisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 Bungeni kwa ajili ya kuangaliwa upya huku kukiwa na mashaka na kupendekeza kufutwa kwa masharti yote 69 ya Muswada huo.

Spika wa Bunge la Taifa ametoa maelezo katika akaunti ya Bunge ya X kuhusu hatua inayofuata baada ya Rais kukataa kutia saini muswada huo.

Mkataba wa Rais unajumuisha kukataa muswada kwa ujumla wake. Athari yake ni kwamba mswada mzima utatupiliwa mbali Bunge la Taifa baada ya Rais kutoridhishwa na mapendekezo yaliyopitishwa katika hatua ya kamati.

"Mjumbe yeyote anayekusudia kukanusha kutoridhishwa/kupiga kura ya turufu ya Rais au kufufua Vifungu vyovyote sitini na tisa (69) vya Muswada anatakiwa kujumlisha kura za angalau theluthi mbili ya Wabunge wa Bunge, wakiwa ni Wajumbe 233. Hii ni kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 115(4)(a) ya Katiba, " hayo ni kwa mujibu wa maelezo ya Spika wa Bunge.

Baada ya kupokea Waraka wa Rais, Spika wa Bunge ameuwasilisha katika Kamati ya Idara ya Fedha na Mipango ya Kitaifa.

Katika maandamano yaliyopinga muswada wa fedha 2024, majengo yaliharibiwa katika sehemu tofauti ya nchi / Picha Reuters 

Mkataba huo uliokataliwa, umepelekwa katika Kamati ya Fedha kwa ajili ya kujadiliwa na hatimae ripoti kufikishwa Bungeni pindi litakapoanza vikao vyake tarehe 22 Julai mwaka huu. Endapo Kamati itashindwa kuripoti Bungeni katika kikao chake kijacho, Bunge litaendelea na kuzingatia Mkataba wa Kamati ya Bunge zima baada ya kurudi kutoka mapumziko.

Suala ambalo limeibua majadiliano kati ya wananchi ni je, Muswada wa Sheria ya Fedha, 2024 unaweza kuwa sheria?

"Kwa msisitizo, hapana! Baada ya kurudishwa bungeni ili kuangaliwa upya kwa sababu, Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 hauwezi kuwa sheria kwa kupitisha muda tu," Spika wa Bunge alifafanua katika akaunti ya X ya Bunge la Taifa la Kenya.

Kwa wiki mbili maandamano yalizuka katika sehemu tofauti nchini Kenya kupinga muswada wa fedha 2024  Picha: AFP 

Je, ni nini athari Ya kukataliwa na kuondolewa kwa mswada mzima wa fedha wa 2024?

"Bunge limetoa muongozo kwamba kukataliwa na kuondolewa kwa Mswada mzima wa Fedha wa 2024 kutasababisha pengo la ufadhili wa takriban Kshs. Bilioni 300 katika matumizi yaliyoidhinishwa na Bunge kupitia Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali, 2024 na makadirio ya mapato yanayoweza kupatikana kutokana na hatua zilizopo za kodi," maelezo ya Spika yamesema.

Mwaka ujao wa Fedha utaanza katika siku nne zijazo, yaani Julai 1, 2024. Chombo kinachoidhinisha fedha kutoka Hazina ya Pamoja kwa ajili ya matumizi ya serikali ya kitaifa ni Mswada wa Matumizi ya Fedha, ambao ni tofauti na Mswada wa Fedha.

TRT Afrika