Mazungumzo hayo yanawaleta pamoja mawaziri, watendaji wakuu katika masuala ya wakimbizi na Makamishna wa mashirika ya wakimbizi. Picha: IGAD sekretariati

Takwimu zaonyesha kuwa kuna takriban watu milioni tano ambao ni wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika eneo la Afrika Mashariki na pembe ya Afrika.

Wale ambao wamelazimika kuhama makwao kwa sababu mbali mbali ni takriban milioni kumi na mbili.

Vyanzo vya kuhama ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi na mizozo.

Mawaziri kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Serikali, IGAD na jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana nchini Uganda kujadili hali ya wakimbizi kandani.

Nchi zinazohusika katika majadiliano ni Burundi, Djibouti, DRC, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Uganda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, na Tanzania.

"Tunahitaji kubadilisha Afrika kwa msaada wa wakimbizi, ndio maana Uganda ni inakaribisha wakimbizi," Hilary Onek Amesema .

Mkutano huo utanfanyika kutoka tarehe 13 had 16 Juni, na una lengo ya kuboresha ulinzi wa kikanda na mazingira ya wakimbizi na jumuiya zinazowapokea.

Pia una lengo la kutafuta njia za kupunguza na kushughulikia vichochezi vya uhamishaji wa wakimbizi katika eneo lote.

Je, hali ya wakimbizi kandani ikoje?

Changamoto kubwa kwa sasa ni ya wakimbizi kutoka nchi ya Sudan ambayo imekumbwa na mzozo tangu mwezi Aprili mwaka huu .

Sudan, ambayo ina rekodi ya muda mrefu ya kuwakaribisha wakimbizi kwa ukarimu, iliwahi kuwa makazi ya zaidi ya wakimbizi milioni 1 - ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika.

Wengi wa wakimbizi walitoka Sudan Kusini, Eritrea, Syria, na Ethiopia, na pia Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad na Yemen.

Mzozo nchini Sudan tangu Aprili mwaka huu umepelekea zaidi ya watu milioni moja kuhepa makwao | Photo Others 

Lakini sasa inakumbwa na changamoto hii ya wakimbizi huku wananchi wa Sudan walkilazimika kukimbia katika nchi jirani za Chad , Sudan Kusini, Ethiopia na Misri.

Shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi, UNHCR linasema zaidi ya watu 800,000 wamekimbia makazi yao ndani ya Sudan. Aidha, zaidi ya wakimbizi 220,000 mkiwemo wakimbizi waliokuwa wamereja nyumbani Sudan wameondoka tena.

Takwimu za UNHCR zaonyesha Kenya imewapa makao zaidi wa wakimbizi 577,492 na wanaotafuta makao, hasa kutoka Somalia, Sudan Kusini na DRC.

Sudan Kusini bado inasalia kuwa nchi kubwa zaidi inayozalisha wakimbizi ikiwa na zaidi ya wakimbizi milioni 2.2 waliokimbilia Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Uganda ina takribani wakimbizi milioni moja na laki tano.

Tanzania inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 246,000 na wanaotafuta hifadhi, hasa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Majadiliano yanalenga mafanikio na mapengo katika ufumbuzi wa kudumu na usimamizi wa wakimbizi.

TRT Afrika