"Wanaume hawapendi kusikia kwamba utazaa zaidi ya mtoto mmoja," Bi. Namukwaya anasema. "Hata baada ya kulazwa, mwanaume wangu hakuwahi kujitokeza."

Safina Namukwaya amekuwa mwanamke mzee zaidi kujifungua barani Afrika baada ya kujifungua mtoto wa kike na wa kiume jioni ya Jumatano tarehe 29 Nov, hospitali ya Women's Hospital International and Fertility Centre katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Madaktari katika hospitali hiyo walisema mama na watoto wake wawili wanaendelea vizuri baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji.

"Hadithi hii sio tu kuhusu mafanikio ya kitabibu, ni kuhusu nguvu na ujasiri wa roho ya binadamu," hospitali ilisema.

Bi. Namukwaya aliambia kituo cha NTV cha Uganda kwamba hii ilikuwa ni mara yake ya pili kujifungua katika kipindi cha miaka mitatu, baada ya kujifungua msichana mnamo 2020.

Mama huyo alisema alipata baadhi ya matatizo na ugumu wakati wa ujauzito wake, ikiwa ni pamoja na baba wa watoto wake kumuacha.

"Wanaume hawapendi kusikia kwamba utazaa zaidi ya mtoto mmoja," Bi. Namukwaya anasema. "Hata baada ya kulazwa, mwanaume wangu hakuwahi kujitokeza."

AFP