kikundi cha ADF kilifanya shambulizi katika shule Ijumaa  / Picha: AFP

Rais Yoweri Museveni amesema mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa Ijumaa na kikundi cha Allied Democratic Forces ni 'ya jinai, ya kigaidi yasiyo namaana.'

" Hasa wakati ambapo serikali ya Kongo imeturuhusu kufanya kazi upande wake wa mpaka, hatuna kisingizio cha kutowawinda magaidi wa ADF hadi tuwamalize," Museveni amesema katika taarifa aliyoweka kwenye mtandawo waTwitter.

" Tutatuma wanajeshi zaidi katika eneo la Kusini mwa mlima Rwenzori ili tuzibe mapengo yoyote," ameongeza Museveni.

Wakati huo huo ulinzi umeimarishwa katika mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, huku watu wakichunguzwa kwa kina na maafisa wa usalama kabla ya kuvuka kila upande.

Mashambulizi ya kigaidi yalifanywa na kikundi cha Allied Democratic Forces, ADF, Ijumaa dhidi ya shule ya upili magharibi mwa nchi.

Ripoti zinasema kuwa wanafunzi 42 waliuawa.

Jeshi la Uganda, UPDF, linaomba wakazi wa eneo hilo kuwa makini.

"Naomba sana tafuteni vijana ambao walielekeza ADF kuja hapa," Meja jenerali Dick Olum, aliwaambia wakazi wa wilaya ya Kasese Magharibi mwa Uganda, kulikotokea shambulio.

Meja Olum ni kamanda wa UPDF wa oparesheni maalum kwa jina 'Shujaa', inayowajibika kukabiliana na wanamgambo wa ADF nchini DRC.

" Waasi walikuja hapa kisiri, wakalala siku mbili ndio wakaja kuchoma watu . walitaka kuchoma magari, wakaona jeshi letu liko karibu wakaogopa, ndipo wakarudi kwa shule" aliongezea, "

" Kwa hivyo kila mtu awe macho, mkiona mtu asiyejulikana akamatwe."

Amesema sio kwamba watu wasiojulikana watafungwa jela, ila tu wahojiwe na viongozi wa eneo kwa ajili ya kubainisha kuwa sio tishio kwa usalama.

Anasema serikali imetuma ndege kwenda kuwasaka waasi hao wa ADF.

''Tunataka kwanza kama inawezekana tuokoe wale wamewashika na kwenda nao,'' ameongeza. Inaripotiwa kuwa wananfunzi sita wakitekwa nyara.

Rambirambi kutoka Umoja wa Afrika

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amelaani mauaji ya wananfunzi yaliyofanywa magharibui mwa Uganda Ijumaa.

"Hakuna maneno ya kuelezea mshtuko wangu kwa mashambulizi hayo , ila kulaani vikali na kuelezea hofu yangu kwa kitendo cha ukikatili na kigaidi cha kikundi cha ADF, kuua wanafunzi," Faki amesema katika taarifa.

" Rambirambi zangu za dhati ziwafikie walioapoteza wapendwa wao katika msiba huo huku nikitoa uhakikisho kuwa niko pamoja na rais Yoweri Museveni na wananchi wa Uganda katika kipindi hiki kigumu kwa taifa," Faki ameongezea.

TRT Afrika