Rais Yoweri Museveni amesema serikali itatumia gharama yoyote kwa wale ambao walipoteza familia zao katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika magharibi mwa nchi Ijumaa iliyopita.
Mashambulizi hayo yalifanywa na kikundi cha Allied Democratic Forces, ADF, na inaripotiwa wanafunzi 42 walikufa.
Wengi walikufa wakati bweni la Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, iliyoko umbali wa chini ya kilomita 2 kutoka mpakani mwa DRC, lilipochomwa moto Ijumaa jioni.
“Rais Museveni ameziagiza wizara zinazohusika kuhakikisha msaada kwa familia zilizofiwa na msiba wa Shule ya Sekondari ya Mpondwe Lhubiriha,” taarifa kutoka ikulu ya Uganda imesema, “ kwa hiyo serikali itasimamia mipango yote ya mazishi, kusaidia waliojeruhiwa, na kutoa msaada wa kifedha."
Jeshi na polisi bado inaendelea kuwasaka magaidi hao katika mbuga ya wanayama ya Virunga ambapo wanaaminika walikimbilia na wanaishi.
Katika taarifa yake kwa mtandawo wa twitter, rais Museveni amesema kuna maswala kadhaa ambayo yanaangaliwa katoika uchunguzi wa mashambulizi hayo,
“Aliyeripoti mara ya kwanza ni nani? Watu waliokuwa karibu hapo walijibu vipi?Mbona watu wetu walio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawakuwa na maelezo kuhusu kundi hili amablo lianonekana lilitawanyika kutoka kwa kundi lao kubwa?”
Museveni amesema majeshi zaidi wanaongezwa katika eneo hilo.
“Tunaleta vikosi vipya kwa upande wa Uganda huku tukiendelea kuwinda magaidi hao upande wa Congo,” ameongezea.