Rais wa Uganda Yoweri Museveni amepimwa na kupatikana na Uviko-19, Jumatano.
Anasema kwa sasa anakabiliwa na dalili ndogo tu, lakini anataka kujitenga kwa muda kwa ajili ya tahadhari.
"Kwa hivyo, nimepata likizo ya pili ya kulazimishwa katika miaka 53 iliyopita, tangu 1971, tulipoanza kupigana na Idi Amin. Wakati mwingine, nilipokuwa na tatizo la ugonjwa wa sinuses ilinibidi nipumzike kwa siku kadhaa ," rais Museveni amesema katika akaunti yake ya Twitter.
" Kama kila mtu anajua, nimekuwa makini sana na Corona, " rais ameongeza , " hata hivyo, hivi majuzi, ilinibidi niache barakoa kwa sababu imekuwa ikisababishia athari za mzio machoni na pia kwenye koo."
Museveni amechanjwa dhidi ya Uviko-19 na wakati wa janga hilo, kila mara alionekana hadharani akiwa amevaa barakoa na kufanya kazi zake rasmi huku akijitenga na watu.