Rais wa Uganda alisema siku ya Jumapili kuwa serikali ya Marekani imekadiria kupita kiasi thamani yake kwa nchi yake baada ya Washington kuamua kuliondoa taifa hilo la Afrika Mashariki kutoka katika mapatano makubwa ya kibiashara kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.
Marekani ilisema wiki iliyopita ilikuwa inaziondoa Uganda pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Gabon na Niger kutoka kwa Mkataba wa Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA) kuanzia Januari 2024.
Mpango huo unatoa ufikiaji bila ushuru katika uchumi mkubwa zaidi duniani kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinakidhi vigezo vya kidemokrasia, ambavyo hutathminiwa kila mwaka.
Katika barua kwa Congress, Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa serikali za CAR na Uganda zote "zimehusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu zinazotambulika kimataifa."
Wanajibeba juu kupita kiasi
Uganda imekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa mataifa ya Magharibi juu ya sheria yake ya kupinga mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa mwezi Mei.
Lakini Rais Yoweri Museveni alikashifu siku ya Jumapili, akiwaambia Waganda "wasiwe na wasiwasi kupita kiasi kutokana na hatua za hivi majuzi za serikali ya Marekani za kushinikiza kampuni zao kusitisha uwekezaji nchini Uganda na kuiondoa Uganda kwenye orodha ya AGOA."
"Baadhi ya wahusika hawa katika ulimwengu wa Magharibi wanajibeba muhimu kupita kiasi na kuwadharau wapigania uhuru wa Afrika," alisema kwenye X, zamani Twitter.
"Kama Uganda inavyohusika, tuna uwezo wa kufikia malengo yetu ya ukuaji na mabadiliko, hata kama baadhi ya wahusika hawatuungi mkono."
Faida 'isiyo na maana'
Msaidizi wake mkuu Odrek Rwabwogo awali alisema kuwa Kampala iko tayari kujadili suala hilo na Marekani, akionya kuwa uamuzi huo utawakumba wakulima wa Uganda na wafanyabiashara wadogo.
"Wakati biashara ya Uganda kupitia AGOA ilikuwa duni, ukuaji wa mauzo yetu kwa Marekani na washirika wengine ulikuwa nguzo muhimu ya mkakati wetu wa kiuchumi kuendelea," Rwabwogo alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano.
Sheria ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ina vifungu vinavyofanya ''ulawiti'' kuwa kosa la kustahiki hukumu ya kifo na inatoa adhabu kwa mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja hadi kifungo cha maisha jela.