Maandamano nchini Msumbiji yaliitishwa na Venancio Mondlane kutoka chama cha upinzani./Picha: Reuters

Mamlaka nchini Msumbiji zimepiga marufuku maandamano yanayoendelea nchini humo toka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Pascoal Ronda alitoa tamko hilo siku ya Ijumaa, huku akiwataka raia wa nchi hiyo kushirikiana na mamlaka "kuzuia machafuko yanayotokana na maandamano hayo."

Akielezea maandamano hayo kama "vitendo vya kigaidi," Ronda alisema: Serikali haitoruhusu maandamano haya yaendelee kuivuruga nchi yetu.”

Siku ya Oktoba 31, Mondlane aliitisha maandamano ya wiki nzima nchini humo, kwa nia ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Mamia ya watu wameitikia wito huo.

Waandishi wa habari wa nje wakamatwa

Waandishi wa habari wawili, Bongani Siziba na Sibonelo Mkhasibe, walikamatwa siku ya Jumatano wakati wakifuatilia maaandamano hayo jijini Maputo.

TRT Afrika