Shambulio la Ijumaa lilionekana kuwa shambulio baya zaidi la wanamgambo katika eneo hilo kwa muda./ Picha : Reuters 

Jeshi la Msumbiji linapambana na wapiganaji wa itikadi kali walioanzisha mashambulizi makubwa katika mji wa kaskazini wa Macomia siku ya Ijumaa asubuhi, Rais Filipe Nyusi alisema katika hotuba yake kwenye televisheni.

Mji huo upo Cabo Delgado, mkoa wa Kaskazini wenye utajiri wa gesi ambapo wanamgambo wenye mafungamano na Deash walianzisha uasi mwaka 2017. Licha ya mwitikio mkubwa wa usalama, kumekuwa na ongezeko la mashambulizi tangu Januari mwaka huu.

"Macomia inashambuliwa tangu asubuhi. Ubadilishanaji wa risasi bado unaendelea," Nyusi alisema karibu saa nne usiku , akiongeza kuwa wanamgambo hao walijiondoa baada ya takriban dakika 45 za mapigano, lakini walijipanga upya na kurejea,'' anaendelea kusema Rais huyo.

Vyanzo viwili vya usalama viliiambia Reuters kwamba mamia ya wapiganaji wanaaminika kuhusika katika shambulio la hivi karibuni.

Shambulio la Ijumaa lilionekana kuwa shambulio baya zaidi la wanamgambo katika eneo hilo kwa muda.

Kikosi cha kikanda kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambacho kilitumwa Msumbiji mwaka 2021, kilianza kuondoka mwezi uliopita huku mamlaka yake yakikamilika Julai.

Nyusi alisema kuwa mashambulizi yanaweza kutokea katika vipindi hivyo vya mpito, na kwamba anatumai vikosi vya SADC vitaweza kuingilia kati na kusaidia.

Rwanda pia imetuma wanajeshi nchini Msumbiji kusaidia kupambana na waasi.

Reuters