Hakuna kipengele cha sheria kuhusu mshauri wa maisha. / Picha: Getty

Na Firmain Eric Mbadinga

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Je, mshauri wa maisha anaweza kukuongoza kwenye mafanikio au furaha? Idadi inayoongezeka ya watumiaji wa mitandao ya kijamii barani Afrika wanaamini hivyo, na wamekuwa wakiwatafuta washauri wa maisha waliojiteua ili kujiboresha kitaaluma na kibinafsi.

Ushauri wa maisha una pande nyingi, unaenea katika kila sehemu ya ustawi wa kimwili na kiroho. Lakini mitandao ya kijamii imeikuza, kuinua ufikiaji, hadhi na malipo ya kifedha ya washauri wa maisha.

Watu hawa wamejishindia idadi kubwa ya wafuasi kwenye mitandao ya Instagram, Facebook, YouTube na TikTok. Na kutokana na uchumaji wa akaunti zao, kuwepo kwenye mitandao ya kijamii kwa muda huamua jinsi makocha hawa wanavyolipwa.

Hata hivyo, mtindo wa biashara wa sekta hiyo unazua maswali kuhusu ubora na ukweli wa baadhi ya maudhui wanazowasilisha.

Mazoea yasiokuwa na maadili

Kando na kuzua mabishano na kuzua gumzo, baadhi ya nasaha zinazotolewa na washauri wa maisha huwaacha wafuasi wao wakiwa katika hatari ya kuathiriwa na mazoea yasiyo ya kimaadili, habari potofu na ulaghai.

Mitandao ya Kijamii iliruhusu washauri wa maisha kujishindia wafuasi wengi. / Picha: AFP

Baadhi ya wachambuzi wanasema baadhi ya makocha wanaozungumza kuhusu nyanja ambazo ni ngumu sana za kiufundi na kisayansi zinaweza kukuza maarifa ambayo hayajakamilika na kueneza habari potofu kati ya wafuasi.

Uthibitisho wa Kitaaluma

Kuna haja ya uthibitishaji bora wa washauri wa maisha na mashirika ya kitaalamu ya kibali, wachambuzi wanasema.

Sylvère Boussamba asema yeye hujiendeleza kiilimu ili abaki kuwa muhimu. Picha : TRT Afrika

Mshauri na mjasiriamali wa Fintech Sylvère Boussamba ni mtu maarufu katika nyanja ya teknolojia ya kompyuta. Kuanzia umri wa miaka 11, alianza ujuzi wa programu ya kompyuta na miaka 40 baadaye alijiimarisha kama mjasiriamali huko Libreville, Gabon.

Ingawa wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii ni wa kawaida ikilinganishwa na washauri wengine wa maisha, hata hivyo, Boussamba ni kocha aliyehitimu na aliyeidhinishwa. Anaangazia sana kufundisha ukuzaji binafsi, ushauri wa kitaaluma na wa kidijitali.

''Nilipata mafunzo katika Chuo cha John C. Maxwell nchini Marekani. Nilitoka kama kocha aliyeidhinishwa, na pia mkufunzi na mhadhiri,” alieleza.

''Hutaacha kujifunza kujihusu, kuhusu watu wengine, kuhusu kile kinachoendelea duniani na kuhusu mbinu mpya na ujuzi mpya, iwe wa kiufundi, usio wa kiufundi au wa mitandao ya kijamii. Kwa hivyo, sehemu ya wakati wangu ni kujitolea kwa kujifunza. Ninajifunza kwenye majukwaa tofauti. Nimejiandikisha katika programu ya ushauri ili kuboresha na kurekebisha njia yangu ya kufanya kazi," Boussamba aliongeza.

TRT Afrika iliwasiliana na baadhi ya washauri mashuhuri wa maisha katika nchi za Afrika zinazozungumza Kifaransa ili kujadili hitaji la viwango na ithibati katika tasnia. Baadhi walikataa kutoa maoni wakitaja sababu za kibinafsi.

Cirille Nyeck anasisitiza ushauri wa maisha unahitaji kufunzwa./ Picha: Afrika

Cirille Nyeck, shemasi Mkatoliki na kocha aliyeidhinishwa kutoka Cameroon, alikuwa miongoni mwa waliokubali kuzungumza juu ya mada hiyo. Kwa anavyoelewa, huwezi kujiboresha na kuwa mshauri wa maisha.

''Ukufunzi uliopangwa unalenga kufikia lengo fulani. Madhumuni na jukumu la mkufunzi ni kuandamana na mwanafunzi wake katika mchakato huu ili kuamua lengo ambalo analolitaja, lengo ambalo ni la kiikolojia, ambalo ni kusema kwamba linazingatia matokeo mazuri na mabaya,"alifafanua.

Nyeck ni mtaarishaji programu wa lugha ya ubongo, ambaye kwa sasa anafanyia kazi tasnifu ya sayansi ya siasa.

Alisema mteja ana rasilimali zote za kufikia malengo yao.

"Ukufunzi ni taaluma inayohitaji sifa na ujuzi mkubwa wa kibinadamu. Unahitaji kufunzwa na kufundishwa vyema kwa hilo," anaongeza.

Uchumaji wa mapato kupitia mitandao ya kijamii

Baadhi ya mipango inayotumiwa na washauri wa maisha kuvutia uchumaji kupitia uwepo wao kwenye mitandao ya kijamii, iwe wamehitimu au la, ni pamoja na kuanzisha akaunti zao za YouTube, Facebook au TikTok nje ya Afrika ili kulipwa vyema na mitandao ya kijamii.

Kwenye TikTok, kwa mfano, video lazima zipokee angalau mara 100,000 ambazo zimetazamwa na akaunti za waandaaji wa maudhui na lazima ziwe na maelfu ya waliojisajili ili kupata pesa.

Masharti ya aina hii husababisha baadhi ya washauri wa maisha wanayotayarisha maudhui kuzingatia kiasi na sio ubora wa maudhui ya video zao, wachambuzi wanasema.

Baadhi ya maneno muhimu ya matangazo yao ni pamoja na "tap, comment, na share na live" - maneno yanayosemwa mara kwa mara kwa wanaofuatilia.

TRT Afrika