Waziri wa Ndani wa Kenya, Kithuri Kindiki atangaza kubuniwa kwa kitengo maalumu kufuatilia mitandao / Picha: Reuters

Waziri wa ndani alitoa tangazo hilo siku ya Jumatano katika bunge la seneti huku akijibu masuali kutoka wabunge.

Aidha Kindiki alikiambia kikao hicho kwamba wapelelezi wanachunguza kikamilifu matukio kadhaa katika kaunti 19, "Tunachunguza kwa kina magenge yanayoendeleza mashambulizi ya ndani na nje ya mtandao dhidi ya Wakenya wanaotoa maoni tofauti kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali."

Aliongeza kuwa washukiwa kadhaa tayari wamefikishwa mahakamani kuhusiana na mauaji ya kikatili ya mwanablogu Daniel Muthiani Bernard, almaarufu Sniper.

Aliwaambia maseneta kwamba wizara yake itahakikisha kuwa Wakenya wanaotumia mitandao kujieleza kwa namna mbalimbali hawatishwi.

TRT Afrika