Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kanda ya Afrika, Dkt Matshidiso Moeti amewapongeza wafanyakazi wa sekta ya afya Rwanda kwa jitihada zao za kupambana na ugonjwa wa Marburg uliozuka nchini humo.
Moeti aliwasili nchini Rwanda siku ya Oktoba 15 kwa nia ya kujionea namna nchi hiyo inavyokabiliana na ugonjwa huo.
“Nimetiwa moyo na namna wafanyakazi wa afya wanavyojitolea kutoa huduma za kinga dhidi ya ugonjwa huu,” alisema Moeti kupitia ukurasa wake wa X.
TRT Afrika