Mhalifu wa Afrika Kusini arejeshwa kwao kutoka Tanzania

Mhalifu wa Afrika Kusini arejeshwa kwao kutoka Tanzania

Thabo Bester alihepa jela Afrika Kusini kwa kugushi taarifa za  kifo chake
Thabo Bester alionekana kujaribu kujificha kama mwenyeji alipokamatwa nchini Tanzania | Picha: Getty Images

Wananchi wawili wa Afrika Kusini Thabo Bester na mpenzi wake Dkt Nandipha Magudumana wamerudishwa Afrika Kusini na mamlaka ya usalama. Waliwasili kutoka Tanzania Alhamisi asubuhi.

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini inasema wawili hao walikamatwa katika mji wa mpakani wa Tanzania wa Arusha. Walikuwa pamoja na raia wa Msumbiji. Watatu hao waliripotiwa kupanga kuvuka hadi Kenya.

Thabo ni mtu ambaye alifungwa kwa madai ya ubakaji na mauaji ,alitoroka jela la Afrika Kusini kwa kudanganya kifo chake.

Mnamo Mei 2022 aliripotiwa kufariki katika seli yake ya gereza katika Kituo cha Marekebisho cha Mangaung huko Bloemfontein, baada ya kuripotiwa kujichoma kwa moto.

Anashtakiwa kwa kuweka mwili ya mtu mwingine katika seli yake na kutoroka.

Uchunguzi mpya ulifunguliwa Machi mwaka huu baada ya utafiti kubaini mwili uliopatikana kwenye seli ya Bester haukuwa wake.Dk Nandipha Magudumanam, mpenzi wa Bester anadaiwa kumsaidia kupanga kifo hicho bandia na kutoroka.

Babake Nandipha na mlinzi wa gereza sasa pia wameshtakiwa kwa kusaidia bester kutoroka ,mauaji na uchomaji moto.

TRT Afrika