Faith Chepchirchir na mwenzake Koech Cheruiyot kutoka Kenya walikuwa wanashindana kwa mara y akwanza kimataifa Picha Tim Olobulu ,( kwa ajili ya TRT Afrika)

Mbio za kilomita kumi zilikamilika kwa kishindo baada ya Adisu Girma kuwaachia kivumbi wapinzani wake na kumaliza kwa dakika 28:52.

Mbio hizo zinasemekana kukumbwa na hali ngumu ya hewa, huku joto na ukungu zikiwavuruga wakimbiaji.

"Ilikuwa ngumu sana kwetu leo, lakini tunafurahi kuvumilia kumaliza mbio. Bila shaka tungetaka kushinda, lakini tunachukua uzoefu na mafunzo,” alisema Koech Cheruiyot (Kenya) baada ya mbio hizo.

Koech alimaliza wa saba kwa kasi ya dakika 30:26.

Adisu Girma alifuatwa kwa karibu zaidi na Tebello Ramakongoana, dakika 28:58 na watatu akawa Moumin Gulleh wa Djibouti kwa dakika 29:05.

Upande wa wanawake haukuleta nafuu yoyote kwa Wakenya hao ambapo wapata nafasi ya tano kupitia Faith Chepchirchir, aliyekimbia kasi ya dakika 34:27.

Ilikuwa furaha kubwa hata hivyo kwa Djibouti baada ya Samiya Hassan Nour kuipatia nchi hiyo dhahabu ya kwanza na kufikisha medali mbili katika mbio hizo upande wa wanawake, alipomaliza kwa dakika 32:18.

Lesotho pia walinyakua medali ya pili ya fedha katika mbiio za kilomita 10 baada ya dada Mokulubete Blandina kupata ushindi wa wanawake kwa dakika 33:15.

Souad Ait Salem wa Algeria alinyakua nafasi ya tatu jukwaani kwa kukimbia kasi ya 33:26.

Koech na Chirchir wa Kenya hawajawahi kushiriki mashindano yoyote nje ya nchi.

''Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza katika mashindano ya kimataifa na nilimaliza nafasi ya tano nikiwa na hali ngumu sana. Tulipambana sana kujaribu kupata matokeo mazuri,” amesema Chirchir baada ya shindano.

Katika shindano lingine timu ya Nigeria iliandikisha medali yake ya kwanza huku Esther Toko akinyakua Shaba katika mchezo wa Makasia.

Shindano la mpira wa mikono lilimalizika kwa ushindi wa wenyeji Tunisia huku Kenya ikichukua fedha Picha : ACNOA ANOCA

Katika mchezo wa mpira wa mkono, Wakenya walinyakua medali ya fedha baada ya kushindwa nguvu na wenyeji Tunisia katika fainali.

Kenya ilifika fainali baada y akuwalaza Mali kwa seti kamili. Awali walikuwa wametishiwa walipochapwa na majirani Uganda lakini wakajikomboa walipokutana na Algeria na kukusanya alama za kutosha.

TRT Afrika