Sébastien Ogier alikaidi agizo la dereva-mwenza Kalle Rovanperä kutimiza ndoto yake ya 1-2-3-4 kwa Toyota Gazoo Racing katika siku ya mwisho ya kuvutia katika Safari Rally Kenya.
Mshindi wa mashindano haya ya kimataifa mwaka jana, 2022 alikuwa Kalle Rovanpera.
Rais wa Kenya William Ruto alimtunukia Ogier na dereva mwenza Vincent Landais vikombe vya ushindi mjini Naivasha.
Kutoka 22 hadi 25 Juni mashindano yalikuwa ya kusisimua kwa wengi waliojitokeza kutazama.
Mashabiki walimiminika kutoka nchini Kenya na wengine kutoka nchi za kigeni
Kulikuwa na timu 20 kutoka nchi tofauti , Kenya iliwakilishwa na timu moja
Ilikuwa pia fursa ya Kenya kujenga utalii , kwani mashindano hayo ya magari yalipita katika mbuga ya wanyama.
TRT Afrika