Picha ya Uwanja wa Ndege wa Uganda. 

Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Tume, Mamlaka za Kisheria na Mashirika ya Serikali (COSASE) nchini Uganda wamehoji uwezo wa wafanyakazi walioajiriwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCCA) kusimamia sekta ya Usafiri wa Anga ya Uganda.

“Afisa mhusika kuwa wafanyakazi waliotajwa huwa wanapandishwa daraja kutoka mafunzo ya kazi, shughuli za kawaida na mikataba, ambayo haihitaji usaili, kwa kuwa tayari wamethibitisha uwezo wao wa kazi. Lakini, sifa ni lazima ziangaliwe na kila wakati zinafaa kulingana na uwezo," Charles Bakabunlindi Waziri wa Wafanyakazi amesema.

"Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefichua kuwa baadhi ya wafanyakazi hao waliajiriwa bila kuzingatia viwango vya msingi vya mahitaji ya kazi na hakuna usaili uliofanyika wakati wa kuajiri," Bakabulindi ameongezea.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alifichua kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda iliajiri wafanyakazi136 kwa mkataba na kudumu na malipo ya kila mwezi ya zaid ya dola 68,000 (Shilingi 254,579,391) bila kutoa ushahidi wa tathmini ya usaili na majalada yao kukosa ushahidi wa maamuzi ya mamlaka husika ya umahiri na sifa za kikazi za watumishi.

“Wafanyakazi 79 waliteuliwa katika nafasi mbalimbali bila kukidhi mahitaji ya msingi ya nafasi hizo, " alibainisha Medard Sseggona mbunge wa Busiro Mashariki wakati akisoma matokeo ya ripoti ya Ukaguzi.

"Uhakiki wa majalada ya wafanyakazi umebaini kuwa mamlaka haijathibitisha wala kuwasimamisha kazi wafanyakazi 9, ambao walikuwa wametumikia kwa muda wa zaidi ya kipindi cha juu cha lazima cha majaribio cha miezi 12," Segona ameongezea

Jennifer Etit, Meneja wa Rasilimali alisema kuwa mamlaka hiyo imewekeza kwa kukuza ujuzi wa wafanyakazi wao wakiwa kazini. Amesisitiza kuwa kuna viwango ambavyo wanazingatia kuwapa watu ajira akidai kuwa kuna wale wanaosita kuongeza ujuzi wao.

“Unaposema kuna viwango fulani unafuata, lakini hapa unasema, vyengine vilikuwa vya kawaida, vyengine havikufuata, vyengine ni kuwahimiza wafanyakazi kufikia kile unachotaka na wanasitasita. Hiyo ina maana kuwa kuajiri hakuna msingi," aliongeza Bakabulindi, Waziri wa Wafanyakazi.

TRT Afrika