Wapiga kura wapatao milioni 17 katika nchi hiyo iliyo kusini mwa Afrika, watamchagua Rais wa nchi yao katika Uchgauzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 9, 2024./Picha: AP       

Wapiga kura wanaokadiriwa kufikia milioni 17 wanatarajiwa kupiga kura hii leo nchini Msumbiji kuchagua viongozi wa nchi hiyo.

Vituo vya kupigia kura vimeanza kufunguliwa mapema saa moja asubuhi na vitakuwa wazi mpaka saa kumi na mbili jioni. Huku matokeo rasmi na ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa baada ya wiki mbili.

Chama tawala nchini humo, cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo kupata uhuru, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine watatu.

Wapiga kura wanaokadiriwa kufikia milioni 17 wanatarajiwa kupiga kura hii leo nchini Msumbiji kuchagua viongozi wa nchi hiyo./Picha: TRTWorldNow

Chapo, anashindana na wagombea wengine watatu huku upinzani mkubwa ukionekana kutoka kwa Ossufo Momade, 63, Mbunge na Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Renamo.

Hofu ya matokeo kuibiwa

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameonyesha wasiwasi iwapo uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa haki, baada ya uchaguzi uliopitwa kugubikwa na madai ya wizi wa kura.

Mwaka 2019, vyama vya upinzani walipinga matokeo ya uchaguzi ambayo Frelimo ilishinda kwa asilimia 73, na kupinga tuhuma za wizi wa kura. Baada ya uchaguzi wa manispaa wa mwaka 2023 kuonekana kama sio haki, maandamano yaliibuka katika miji mikubwa ambapo polisi, kwa kile kinachodaiwa ni bahati mbaya, waliua watu kadhaa.

SADC yatuma salamu za heri

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika), ameitakia Msumbiji Uchaguzi Mkuu mwema.

Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika), Samia Suluhu Hassan./Picha: Ikulu Tanzania

Rais Samia amewataka raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato huo, ambao pia ni haki yao ya msingi ya kidemokrasia.

Wapiga kura wapatao milioni 17 katika nchi hiyo iliyo kusini mwa Afrika, watamchagua Rais wa nchi yao katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 9, 2024.

Msumbiji inafanya uchaguzi wake wa saba tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1975.

TRT Afrika