Magari ya kijeshi na magari ya kubeba wanajeshi yalishika doria barabarani na askari wenye silaha nzito wakiwasaidia polisi kuzuia uporaji na uharibifu | Picha: Reuters

Jaji Lawrence Mugambi alisema kuendelea kwa jeshi kusaidia polisi ni muhimu kutokana na hitaji la kudumisha amani na usalama wa umma na kulinda miundombinu muhimu.

"Kutokana na kuzuka kwa vurugu na kupoteza udhibiti wa polisi wakati wa maandamano, hali iliyolazimu kupelekwa kwa KDF ambayo ilihatarisha maisha na mali, matumizi ya kifungu cha 241(b) yalitumiwa ipasavyo katika hali hizo," alisema.

Jaji alisema kuwa ingawa hatua hiyo ilikuwa na haki, ilikuwa wazi kwamba umma haukujulishwa kikamilifu kuhusu kiwango cha ushiriki na uhusishaji wa jeshi.

Alikubaliana na Chama cha Wanasheria cha Kenya, LSK, kwamba kupeleka KDF kwa njia hiyo ni hatari ambayo unaweza leta utawala wa kijeshi katika nchi.

Kwa msingi huu, LSK ilimwambia Jaji Mugambi kwamba hakuna taarifa kutoka kwa serikali kuhusu kama uwepo wa jeshi katika mji mkuu unalenga kushughulikia dharura au kushughulikia machafuko au hali ya kutokuwa na utulivu.

TRT Afrika