Kenya's Defence Minister Aden Duale deployed the military to contain tax hike protests on June 25, 2024./ Photo: AFP

Waziri wa Ulinzi wa Kenya Aden Duale ametangaza kuwa wanajeshi wametumwa kusaidia polisi kuzuia maandamano baada ya maandamano mabaya ya ongezeko la ushuru kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya nchi siku ya Jumanne.

Katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa Jumanne usiku, Duale alisema Vikosi vya Ulinzi vya Kenya "vitaunga mkono huduma ya polisi ya kitaifa katika kukabiliana na dharura ya usalama iliyosababishwa na maandamano ya ghasia yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Kenya na kusababisha uharibifu na uvunjaji wa miundombinu muhimu. "

TRT Afrika