Mahakama ya Afrika yaipa Kenya miezi 3 kutekeleza amri kuhusu jamii ya Ogiek

Mahakama ya Afrika yaipa Kenya miezi 3 kutekeleza amri kuhusu jamii ya Ogiek

Amri hiyo ilitolewa na AfCHPR siku ya Novemba 12, jijini Arusha, Tanzania.
Jamii ya Ogiek ambao ni wawindaji kiasili, inakadiriwa kuwa ni jumla ya watu 45,000m huku wakitegemea zaidi msitu wa Mau nchini Kenya kama uhai wao. @OgiekPeoples    

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeipa serikali ya Kenya miezi mitatu kuipa mahakama hiyo mrejesho wa utekelezwaji wa maamuzi ya keshi namba 006/2012 iliyotolewa na hiyo inayoketi jijini Arusha, nchini Tanzania.

Mahakama hiyo, pia iliitaka Kenya kutengeneza sera maalumu za kuilinda jamii asili ya Ogiek nchini humo.

Mwezi Mei mwaka 2022, Mahakama ya AfCHPR ilibaini kuwa serikali ya Kenya ilikiuka haki ya kuishi, kumiliki mali, maliasili, maendeleo, dini na utamaduni wa jamii ya Ogiek, kwa mujibu wa Katiba ya Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeipa serikali ya Kenya miezi mitatu kuipa mahakama hiyo mrejesho wa utekelezwaji wa maamuzi ya keshi namba 006/2012 iliyotolewa na hiyo inayoketi jijini Arusha, nchini Tanzania./Picha: Wengine

Kwa upande wake, serikali ya Kenya iliomba kuahirishwa kwa usikilizwaji wa shauri hilo, ili iweze kuwasilisha baadhi ya hatua za utekelezwaji wa hukumu hiyo.

Jamii ya Ogiek, ambao ni wawindaji kiasili, inakadiriwa kuwa ni jumla ya watu 45,000m huku wakitegemea zaidi msitu wa Mau nchini Kenya kama sehemu ya uhai wao.

Hata hivyo, jamii hiyo imekuwa ikiondolewa nje ya msitu huo na maofisa uhifadhi KFS na KWS.

TRT Afrika