Maandamano yanafanyika katika sehemu tofauti nchini Kenya/ Picha : Reuters

Maandamano katika sehemu tofauti nchini Kenya yanafanyika huku vijana wa Gen Z wakiendelea kupinga serikali ya Rais William Ruto.

Maandamano yalianza Juni mwaka huu kwa ajili ya kupinga muswada wa fedha 2024, lakini hata baada ya Rais Ruto kukataa kutia saini muswada huu, waandamanaji waliendelea kupinga serikali ya Rais Ruto.

Wandamanaji wanaipinga serikali ya rais William Ruto/ Picha: Reuters 

"Ikiwa huwezi kushiriki katika maandamano, kaa nyumbani kwa kumbukumbu ya mashujaa tuliopoteza katika maandamano ya amani, na kwa mshikamano na Gen Zs ambao wanapigania Kenya bora. #RutoMustGo," ameandika mwanaharakati maarufu nchini Kenya, Boniface Mwangi katika akaunti yake ya X.

Baadhi ya vijana nchini Kenya wameingia mitaani wakidai mabadiliko ya uongozi nchini humo.  / Picha: AFP

Polisi imepinga maandamano hayo ikisema haijatoa kibali cha kwa waandamanaji.

"Maandamano ya amani yanalindwa kikatiba nchini Kenya. Hakuna mtu anayepaswa kuiondoa kutoka kwako. Wakati haki hii inashambuliwa, itetee," Tume ya Haki nchini Kenya imesema.

Polisi wameonekana wakitumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji/ Picha: AFP 

Katika mji mkuu wa Nairobi polisi wameonekana wakitumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji huku wengine wakionekana kutawanywa na wengine wamejeruhiwa.

Baadhi ya waandamanaji wakiingizwa katika gari ya polisi. / Picha AFP

Rais William Ruto amefanya marekebisho kadhaa katika serikali yake akijitahidi kutimiza matakwa ya vijana ambao wameonyesha kutofurahishwa na serikali yake.

Kwa mfano amewafuta kazi makatibu wa baraza au mawaziri wote 21 pamoja na mwanasheria mkuu akisema kuwa anataka kuunda serikali ndogo zaidi na itakayomuwezesha kutimiza ahadi yake kwa Wakenya.

Katika mji wa Kajiado waandamanaji wameziba barabara/ Picha: Reuters 

Wiki hii rais William ruto alikuwa amependekeza kuwe na majadiliano na vijana na maongezi ili kuelewa suluhisho la kutoridhishwa kwao na serikali.

Wazo hili liliungwa mkono hadharani na kiongozi wa muungano wa Chama cha Azimio Raila Odinga. Hata hivyo, vijana kupitia mitandao ya kijamii walimuambia kuwa hawamtambui kama muakilishi wao na hawataki maongezi, wanachotaka ni mabadiliko katika uongozi wa nchi.

Maandamano yanayofanyika Kenya hayana kiongozi , vijana huwasiliana kupitia mitandao ya kijamii/ Picha : Reuters 
TRT Afrika