Viongozi wa Afrika wanaohudhuria Wiki ya Uendelevu ya Abu Dhabi ya 2025 (ADSW) wamehimiza kuwepo kwa mazungumzo yenye matokeo zaidi, ushirikiano, fursa za uwekezaji, na ushirikiano wa heshima kati ya mataifa ya Afrika na jumuiya ya kimataifa.
Wiki ya Uendelevu ya Abu Dhabi (ADSW) ilizinduliwa mwaka wa 2008 kama "jukwaa la kimataifa kwa wote ambao wana hisa katika siku zijazo za sayari yetu," tovuti ya tukio hilo inasema.
Pia inalenga "kuonyesha jinsi muunganiko wa teknolojia za hali ya juu, ikijumuisha akili bandia (AI), nishati, na utaalam wa binadamu, unavyoweza kuongeza kasi ya maendeleo endelevu na kufungua fursa ya mabadiliko ya kiuchumi ya Dola trilioni 10 za Marekani.
Kongamano la mwaka huu, linalofanyika kuanzia Januari 12-18 chini ya uangalizi wa Rais wa UAE Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, linalenga "kuharakisha maendeleo endelevu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi''.
'Mijadala isiyo na mwisho'
Imeleta viongozi wengi kutoka duniani kote, ikiwa ni pamoja na Afrika kadhaa. Viongozi wa Afrika walikariri haja ya jumuiya ya kimataifa kujitolea tena kwa ajenda ya kimataifa ya uendelevu.
Pia walisisitiza haja ya juhudi kubwa zaidi ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi, ushirikishwaji wa kijamii, na ulinzi wa mazingira, hasa kwa mataifa yanayoendelea ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa - shida ambayo mara nyingi huchochewa na hatua za mataifa yaliyoendelea.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alionyesha kuchoshwa na pengo kati ya ahadi za kisiasa za vikao vya zamani na hatua madhubuti katika taarifa yake juu ya X.
"Ajenda ya kimataifa ya uendelevu kama ilivyo bado haijatekeleza ahadi yake, hasa kwa Afrika," Kagame alisema.
“Ahadi za kisiasa hazifikiwi kwa vitendo, hivyo kutuacha na mijadala isiyoisha na kunyoosheana vidole. Ili kufikia malengo yote mawili, tunapaswa kutumia teknolojia ya bei nafuu, inayoweza kubadilika na yenye manufaa kiuchumi,'' alisema.
Fursa za kiuchumi
Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa UAE, Dk. Sultan Al Jaber, akiangazia jukumu la ADSW katika kuwezesha miunganisho ya biashara.
"Wiki ya Uendelevu ya Abu Dhabi 2025 itafanya kazi kama kiunganishi cha viongozi wa biashara duniani kote, watunga sera, na wafanyabiashara, kwa kutumia masuluhisho yaliyounganishwa ambayo yanajenga mustakabali mzuri zaidi kwa wote," Al Jaber alisema katika hotuba yake ya ufunguzi.
Rais wa Kenya William Ruto pia alisifu fursa ambazo kongamano hilo linawasilisha, akitolea mfano mkataba mpya wa kiuchumi kati ya nchi yake na UAE uliotiwa saini kando ya mkutano huo.
''Tunachunguza makubaliano ya ushirikiano na Umoja wa Falme za Kiarabu kupanua Reli ya Standard Gauge kuunganisha Kenya, Uganda na Sudan Kusini,'' Ruto alisema.
''Kama sehemu ya mpango huo, tumekubali kufanya upembuzi yakinifu juu ya upanuzi wa SGR kutokana na uwezo wake wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kukuza biashara,'' aliongeza.
"Wakati wa Afrika"
''Inatarajiwa kuongeza zaidi ya mara tatu mauzo ya Kenya ya bidhaa za nyama, matunda, mboga mboga, maua yaliyokatwa, chai na kahawa mara itakapotekelezwa," Rais wa Kenan aliongeza.
Hata hivyo, mada ya mara kwa mara ya ahadi ambazo hazijafikiwa na ukosefu wa uwakilishi sawa katika meza ya mazungumzo ya kimataifa imesalia kuwa wasiwasi mkuu kwa viongozi wa Afrika.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu alisisitiza umuhimu wa kujitegemea na ushirikiano wa ndani ya Afrika.
''Afrika ina kile inachohitaji kujiendeleza. Tuna rasilimali, watu na uwezo. Ni lazima tuangalie ndani ili kuboresha biashara na ushirikiano wa ndani ya Afrika ili kuwanufaisha watu wa Afrika na bara. Wakati wa Afrika ni sasa,” Tinubu alisisitiza katika taarifa yake.