Licha ya wataalamu walioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuthibitisha kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu bado unafanywa nchini Ethiopia, uchunguzi ulioanzoishwa kutokana na vita vya miaka miwili huko Tigray unakabiliwa na kufungwa. / Picha: Reuters 

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilishutumu kule kutochukuliwa hatua kwa uchunguzi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu madai ya ukatili nchini Ethiopia kama "usaliti mbaya" wa wahasiriwa na jumuiya ya kimataifa.

Mamlaka ya wataalam wanaochunguza matukio hayo yatakamilika wiki ijayo baada ya nchi wanachama katika kikao cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kushindwa kuwasilisha rasimu ya azimio la kurefusha muda huo.

Hii ilifanyika licha ya ripoti mbaya kutolewa na Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu nchini Ethiopia (ICHREE) iliyo onya kuhusu "hatari kubwa" ya ukatili zaidi huko.

Nchi wanachama wa baraza la haki "zilizima njia pekee ya kuaminika ya uchunguzi huru wa kimataifa na uangalizi juu ya Ethiopia - chanzo kikuu cha matumaini kwa waathiriwa na waathirika wanaotafuta haki na uwajibikaji," ilisema Amnesty.

"Uamuzi wa kutoendelea na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukwaji wa haki unaoendelea, huku kukiwa na hali ya hatari ya kitaifa na maonyo ya ICHREE ni usaliti mbaya kwa wahasiriwa na walionusurika," iliongeza.

"Uamuzi wa EU wa kupuuza maonyo ya Umoja wa Mataifa na kuachana na utaratibu pekee huru, unaoaminika wa kimataifa wa uchunguzi kuhusu Ethiopia ni aibu," Amnesty ilisema.

IHREE ilianzishwa mnamo Desemba 2021, kwa ombi la Umoja wa Ulaya, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita vya kikatili katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray.

TRT World