Nchi kadhaa za Kiafrika zimethibitisha hivi karibuni maambukizi ya Mpox. Picha / Reuters

Na Firmain Eric Mbadinga

Ugonjwa wa Mpox unaosababishwa na virusi vya familia moja na maradhi ya ndui unatishia kuenea barani Afrika kutokana na mlipuko huo mkubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kulingana na takwimu rasmi, karibia watu 19,000 katika nchi 12 za bara wameambukizwa na maradhi ya Mpox hadi sasa.

Wakati Kongo inasalia kuwa fokasi wa aina mpya ya "Clade Ib", kuenea kwa ugonjwa huo katika nchi nyingine 11 za Afrika kunatia wasiwasi mkubwa.

Wiki chache zilizopita, wakala wa huduma ya afya wa Umoja wa Afrika, Afrika CDC, iliripoti kwamba kiwango cha Mpox tangu kuripotiwa kwa maambukizi ya kwanza ya binadamu iliporekodiwa mwaka 1970 iliongezeka na kuwa janga lililotarajiwa kuenea, hasa katika bara hilo.

Kwa hivyo, mashirika ya huduma ya afya yanasimama wapi kuepusha kile ambacho Afrika na dunia nzima imeshindwa?

Wataalamu kama vile Dk Jean Vivien Mombouli kutoka Kongo wanaamini kwamba mkakati uliotumiwa kukabiliana na virusi vya Ebola barani Afrika ni kielelezo kinachofaa kuigwa.

Mafunzo ya Ebola

Mlipuko wa mwisho wa Ebola barani Afrika ulidhibitiwa mnamo 2022 nchini DRC, Dk Mombouli akiwa mmoja wa walio mstari wa mbele wa kutoa matibabu katika nchi yake ya asili na Guinea, ambapo ugonjwa huo ulisababisha vifo vya watu 2,500 kati ya 2013 na 2016.

Chumba cha dharura ambacho Dkt Mombouli alikuwa sehemu yake kilishirikiana na chumba cha dharura huko Kinshasa katika mchakato wa pamoja wa kukabiliana na maambukizi hayo wakati wa kilele cha mlipuko huo.

Kama mtaalamu wa fiziolojia ya molekuli na famasia, anaamini kwamba hatua za mapema ni muhimu ikiwa bara litazuia kuenea kwa virusi vya Mpox.

"Tulianzisha uchunguzi sambamba wa afya ya binadamu na wanyama ili kuweka mipaka ya maeneo ya misitu ambapo virusi vingeenea kwa mwaka mmoja. Pia tulitekeleza mikakati kama hiyo ili kulimaliza janga hili nchini Guinea," Dk Mombouli anaiambia TRT Afrika.

Huko Kivu Kaskazini mwa Kongo, ambako Ebola ilikuwa ikiendelea kwa miaka miwili, timu ya kukabiliana na ugonjwa huo ilinufaika na utaalamu wa Prof Jean-Jacques Muyembe, mwanabiolojia wa mikrobiolojia ambaye aligundua virusi vya Ebola mwaka wa 1976 na kwa sasa ni mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Kitaifa ya Matibabu ya DRC.

Kulingana na ushauri wa Muyembe, warsha zilizohusisha wataalamu, maafisa wa kijeshi na wengine ziliandaliwa ili kuandaa mkakati madhubuti kwa maeneo ambayo virusi hivyo vimekuwa vikisambaa.

Warsha hizo ziliwezesha uratibu bora wa afua za afya ya umma, na kuongeza kasi ya kuzuia janga hili.

Mpox, ambayo hapo awali ilijulikana kama 'Monkeypox, inaweza kutibiwa kupitia chanjo. Picha: Reuters

"Mbali na mikakati iliyoratibiwa na juhudi za pamoja ili kudhibiti virusi kama Mpox, ni muhimu kuongeza ufahamu wa ugonjwa huo, asili yake na njia ya maambukizi.

Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba kuna njia mbili ya maambukizo ya Mpox - kupitia wanyama, kupitia binadamu na maambukizi ya ngono kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu mwengine,'' anaeleza Dk Mombouli.

Kutegemea chonjo

Nchini DRC, kumekuwa na angalau vifo 500 kutoka kwa waathiriwa 14,000 wanaoshukiwa kuambukizwa tangu kutokea kwa aina mpya.

Mamlaka ya Kongo inalenga kuongeza juhudi za ukabilianaji wa dharura ya afya ya umma kwa dozi milioni 3.5 za chanjo ya Mpox.

Katika mkutano na wanahabari wiki jana, waziri wa afya Samuel-Roger Kamba alisema serikali inakusanya rasilimali zote zilizopo kununua chanjo. Pia alitangaza kwamba Marekani ilikuwa imeahidi dozi 50,000 za kwanza, wakati Japan ilikuwa imetoa dozi milioni tatu kwa watoto.

Tangazo la Shirika la Afya Duniani la "dharura ya afya ya umma na wasiwasi wa kimataifa" katikati ya Agosti inatarajiwa kuchochea utoaji wa chanjo kwa nchi zingine zilizoathiriwa katika bara hilo. Mbali na Bonde la Kongo, ugonjwa huo umeenea hadi Burundi, Côte d'Ivoire, Thailand, Afrika Kusini, Nigeria, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mpox inajulikana kusababisha vifo vingi kati ya watu walio na mfumo wa kinga dhaifu. Pia kuna upotezaji wa kuona. Katika baadhi ya matukio, uharibifu wa uso hutokea.

Maambukizi haya ya magonjwa yote ni sehemu ya aina ya 'Clade Ib' inayoweza kuenea kwa kasi.

"Tuko katika hatua ya awali, tunahitaji nchi zilizoathirika kukusanya rasilimali kabla ya wakati. Kwa kuwa Mpox inaenea polepole zaidi kuliko Ebola, itatuwezesha kuzuia kuenea kwa maradhi hayo katika Afrika Magharibi na nchi za Bonde la Kongo, ikiwa ni pamoja na Angola," alisema. Zambia, Sudan Kusini na Chad," anasema Dk Mombouli.

TRT Afrika