mbegu ya pamba imetolewa kwa wakulima katika kaunti ya Busia /Picha/ Hussein Mohamed mseamji wa Rais wa Kenya 

Serikali ya Kenya itawapa wakulima wa pamba tani 17 za mbegu za pamba aina ya BT Cotton katika County ya Busia, magharibi mwa nchi.

"Jumla ya Wakenya 12,000 wamesajiliwa kama wakulima wa pamba," Hussein Mohamed, msemaji wa rais William Ruto amesema.

Eneo hilo la Busia linalenga kupanda jumla ya ekari 11,253 ya pamba katika awamu ya kwanza.

"Katika kaunti hii , serikali inanuia kutenga ekari 42,000 za ardhi chini ya uzalishaji wa pamba," Mohammed amesema katika taarifa.

Mpango wa serikali ni kuzalisha kilo 800 kwa kila ekari ya nyuzi za pamba na mashuhudu ya pamba (cotton cake) - Yaani mabaki ya mbegu za pamba baada ya kukamuliwa mafuta ambacho hutumiwa kama chakula cha ng'ombe.

Hii ni sawa na zaidi ya kilo milioni tisa; kilo milioni tatu za pamba na kilo milioni sita za keki ya mbegu ya pamba.

Februari mwaka huu bunge la Kenya liliwakilisha mswada wa sheria yenye nia ya kufanya maendeleo katika sekta ya pamba nchini.

Kwa sasa, uzalishaji wa pamba nchini Kenya unafikia marobota 28,000 kila mwaka, chini sana kuliko marobota 140,000 yanayohitajika.

Ili kuziba pengo hili, makampuni yanategemea uagizaji bidhaa kutoka nje kwa 80% ya malighafi, ambayo kimsingi inatoka India, Uchina, na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

TRT Afrika