Mahakama ya Kenya imewakilisha mbele ya bunge la taifa Miswada ya kubadilisha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Miswada hiyo- Mswada wa Sheria ya Kanuni za Adhabu (Marekebisho) ya Sheria ya 2023 na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Marekebisho) 2023, inalenga kupunguza vifungo vya wauaji, wahalifu wa ngono na wale wanaokabiliwa na kifungo cha maisha hadi miaka 30.
"Hii ni hatua muhimu katika safari ya taifa letu kuelekea mageuzi ya haki ya jinai," jaji mkuu Martha Koome amesema.
Pia inalenga kukomesha hukumu ya kifo nchini Kenya.
"Miongoni mwa vifungu muhimu vya mswada wa sheria ya Kanuni za Adhabu (Marekebisho) 2023 ni kutetea ushirikishwaji kwa kutumia 'lugha rafiki' kwa haki za binadamu, hasa kuhusu ndugu na dada zetu wenye ulemavu wa kiakili na kisaikolojia," Koome amesema.
Sheria ambayo Kenya inatumia sasa ilitungwa miaka ya 1930, wakati Kenya ilikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.
Inasema kwamba mtu anaweza kuhukumiwa kifo ikiwa atapatikana na hatia ya mauaji, wizi wa kutumia mabavu au uhaini.
Mahakama inataka neno ‘kifo’ lifutwe na badala yake iwekwe ‘kifungo cha maisha jela.’
"Mabadailoko yanasimamia haki na utu wa watoto wetu, ikiondoa masharti ya zamani ambayo yanawafunga kwa hatua zisizofaa za adhabu," jaji mkuu Koome ameelezea zaidi.
Mabadailiko yatakapopitishwa kuwa sheria, Kenya itaungana na mataifa mengine ishirini na sita ya Afrika, ambayo yamekomesha hukumu ya kifo kisheria.
Hizi ni pamoja na Cape Verde, Chad, Sierra Leone, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ghana na Zambia,
"Kwa hiyo, adhabu ya kifo kama aina ya adhabu ndani ya mfumo wa haki ya jinai nchini Kenya itakuwa ni historia, ikiwa imefutwa kabisa kutoka kwa sheria yetu." taarifa kutoka Tume ya kimataifa ya mahakimu, ICJ.
Tume hii ya wataalam wa sheria linaongezea,
"Njia za utekelezaji zenyewe zinaweza kusababisha maumivu ya kipekee kwa mtu kabla ya kutangazwa kuwa amekufa, kama vile sio tu kuwa ukatili bali pia ni unyama."