Moody's ilipunguza ukadiriaji wa Kenya na 'kuibwaga mapipani,' ikitaja kupungua kwa uwezo wa kutekeleza mkakati wa ujumuishaji wa kifedha ili kudhibiti mzigo wake wa deni.
Wakala wa ukadiriaji wa mikopo ulishusha daraja la ukadiriaji wa watoaji wa muda mrefu wa ndani na nje ya nchi na viwango vya juu vya deni lisilolindwa hadi "Caa1" kutoka "B3".
Mnamo mwezi Juni, Rais wa Kenya Willian Ruto aliondoa mpango wa kupandisha ushuru ili kukabiliana na maandamano makubwa ambayo yalisababisha vifo vya watu 24.
Mswada wa fedha uliotupiliwa mbali ulikuwa na hatua zilizokusudiwa kusaidia lengo la serikali kukusanya dola bilioni 2.7 katika ushuru wa ziada ili kupunguza nakisi ya bajeti na ukopaji wa serikali.
Ili kufidia mswada wa fedha ulioondolewa, utawala wa Ruto umependekeza kupunguzwa kwa matumizi.
Moody's ilisema kuwa ingawa upunguzaji wa matumizi unapaswa kupunguza nakisi ya fedha, itakuwa katika kasi ya taratibu zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali, na matokeo yake kutarajia uwezo wa kumudu deni la Kenya kubaki dhaifu kwa muda mrefu.
Kwa ujumla, ukadiriaji wa mikopo hutumiwa na mifuko ya mamlaka ya serikali, mifuko ya pensheni na wawekezaji wengine ili kutathmini ubora wa mkopo wa Kenya hivyo kuwa na athari kubwa kwa gharama za kukopa nchini.