Kenya imerejesha ruzuku ya petroli ambayo ilifutwa miezi kumi na moja iliyopita na Rais William Ruto baada ya kusema kuwa serikali haiwezi kudumu.
Kenya inakabiliwa na gharama kubwa ya chakula na mafuta na hatua ya ruzuku inakuja kufuatia ongezeko la ushuru ambalo lilizua maandamano makubwa.
Katika taarifa, mdhibiti wa nishati alisema ruzuku hiyo itatumika kufidia kampuni za uuzaji wa mafuta.
Inamaanisha kuwa bei za petroli zitasalia bila kubadilika kwa mwezi mmoja hadi Septemba 14.
Kulinda wateja
"Ili kuwapa afuo wateja kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na kuongezeka kwa gharama , serikali imechagua kuleta utulivu wa bei za pampu kwa muda wa bei wa Agosti-Septemba," mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli ilisema.
Serikali mwezi uliopita iliongeza maradufu ushuru wa ongezeko la thamani kwabei za mafuta hadi 16% katika sheria ambayo pia ilianzisha ushuru wa nyumba wa 1.5% kwa wafanyikazi wote na kupandisha kiwango cha juu cha ushuru wa mapato ya kibinafsi hadi 35%.
Sheria hiyo inapingwa mahakamani.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Ruto alisema kuwa ruzuku hiyo imekuwa ya gharama kubwa na inaweza kutumika vibaya, ikiwa ni pamoja na kusababisha upungufu bandia.
Hii ilikuwa baada ya wizara ya fedha kusema Kenya inaweza kukosa fedha za kufadhili gharama ya mafuta ikiwa bei itaendelea kupanda.