Na Sylvia Chebet
'Tembea pole pole kama mzee Kobe', unaweza ukawa msemo uliojipatia umaarufu. Hata hivyo, hali ni tofauti kwa kiumbe hiki kidogo.
Kikiwa kinafahamika kwa kasi yake, kiumbe hiki kinapatikana sana katika ukanda wa Afrika Mashariki, hasa katika nchi za Kenya na Tanzania.
Kutokana na kuwa na mashimo kwenye mgongo wake, Kobe hawa huwa ni wepesi hasa wanapowakimbia maadui zao.
Ganda hilo humfanya atambae kirahisi na kujificha kujificha kwenye mapango.
Sifa hizo hizo, ndizo zinazowafanya iwe rahisi kwao kujificha, pindi wanapohisi hatari yoyote.
Upekee wa mwili wake hufanya kiumbe hiko kuwa bidhaa inayomezewa mate sana, na kuweka mustakanbali yake hatarini.
Kobe hao husafirishwa kwa magendo katika nchi tofauti "ambako wanatumika kama wanyama wa kufugwa, lakini pia katika baadhi ya nchi, wanaliwa kama kitoweo, hasa katika bara la Asia," Meneja katika Shirika la Wanyama Duniani, Edith Kabesiime anaiambia TRT Afrika.
Wanatumika kama wanyama wa ndani katika baadhi ya nchi za Magharibi huku wengi wakivutiwa na udogo wao na mwonekano wao wa kupendeza.
Kiumbe huyu mwenye kuvutia ni kati ya wanyama wenye kuhitajika sana ulimwenguni kati ya wanyama watambaao zaidi ya 500 na aina 500 za ndege wanaouzwa kote ulimwenguni, kulingana na Shirika hilo.
Wahifadhi wanasema kuwa viumbe hao huwekwa kwenye nyumba za watu tofauti na sehemu zao asili.
"Biashara ya wanyamapori duniani kote ni kubwa sana. Kutoka Afrika, haifikiriki na bila shaka, hiyo ni sababu kubwa kwa nini Afrika inapoteza urithi wake wa wanyamapori," Kabesiime anasema kuhusu sekta ya mabilioni ya dola.
Katika eneo korofi katika kaunti ya kaskazini mwa Kenya ya Marsabit, macho ya Simon Mwangi yanaangazia eneo kubwa lenye ukame, akitafuta ishara yoyote ya kiumbe huyo ambaye haonekani kuwa rahisi.
Muhifadhi huyo mzoefu anaweza kuwoana viumbe hao kutoka umbali wowote, iwe katika miamba hata jangwani.
Macho yake ya kitaalam huona viumbe hawa wakisogea karibu na nguzo za mawe hadi kwenye nyufa.
Anapotoa mikono yake, wanamkumbatia kwa upole kobe mdogo na ganda bapa ambalo hujificha kwa mazingira ya mawe.
“Hii ni fursa adimu sana,” Mwangi analiambia Shirika la Habari la Anadolu HUKU akiendelea kuwakagua Kobe hao.
“Yatupasa kufanya kila liwezekanalo kuwalinda viumbe hawa.”
Taasisi ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Asili (IUCN) imewaorodhesha viumbe hao kama walio hatarini kutoweka.
Kobe hawa wadogo, wanaopatikana katika sehemu zenye uoto wa savanna na sehemu kame zenye joto katika ukanda wa Afrika Mashariki, hutegemea sana miamba kama sehemu zao kujihifadhi.
Hata hivyo, viumbe hao wanapitia changamoto ya kukosa makazi yao ya asili. Wataalamu wanasema kuwa maendeleo katika shughuli za kilimo yanamaliza maeneo asilia ya viumbe hawa, mengi yakiteketezwa kwa moto.
Kwa upande wa Tanzania, Kobe wadogo wanakosa makazi kutokana na ufugaji wa mifugo kupita kiasi na shughuli zingine za binadamu.
Wakati ukuta
Mwaka 2018, IUCN ilisema kuwa kumekuwepo na upungufu wa takriban asilimia 80 ya viumbe hao katika miongo mitatu.”
Mwenendo huwa unatarajiwa kuendelea kwa miaka 15 ijayo, na hivyo kuwafanya Kobe wadogo kuwa viumbe walio hatarini zaidi,” kulingana na ripoti hiyo.
Kwa kuzingatia hilo, Kenya imeanzisha juhudi za kiuhifadhi zinazolenga kuwalinda viumbe hao, ingawa wataalam wanasema kuna mengi zaidi ya kufanya.
Juhudi hizo ni pamoja na kuainisha maeneo ya mtawanyo na makazi ya viumbe hao katika kaunti kame za Kenya zikiwemo Marsabit, Samburu, Isiolo, Laikipia, na Meru.
Wataalamu wanapendekeza hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kudhibiti ujangili, taratibu za ulinzi kwa makazi yao ya asili na kuanzisha kampeni za uhamasishaji wa uhifadhi miongoni mwa jamii za wenyeji.