Kenya itaanzisha bima mpya ya afya kuanzia mwezi Machi mwaka huu. / Picha kutoka Kenyatta Hospital Kenya

Wizara ya afya ya Kenya iko mbioni kuanzisha mfumo mpya wa huduma ya bima ya afya, inayotarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu.

Huduma hiyo itajulikana kama mfuko wa bima ya afya kwa jamii (Social Health Insurance Fund), ikichukua nafasi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (National Health Insurance Fund (NHIF), unayotumika kwa sasa.

"Matarajio yetu kama wizara ni kwamba ifikapo Machi 1, 2023, tunapaswa kuanza usajili wa kila mtu katika huduma hii mpya ambapo wanachama wataanza kulipia huduma kupitia makato yatokanayo na mishahara yao ya kila mwisho wa mwezi,” alisema waziri wa afya Wafula Nakhumicha.

Serikali inasema mfumo huo mpya ni hatua ya kuelekea kufikia mfumo wa afya jumuishi zaidi na unaoweza kufikiwa nchini Kenya.

"Asilimia 54 ya Wakenya watafaidika na michango iliyopunguzwa ya NHIF," anaeleza Isaac Mwaura , msemaji wa serikali ya Kenya.

Tofauti ya Mifuko hiyo

" Awali, wanufaika wa mfuko wa zamani walitenga asilimia 5 ya mishahara yao kwa michango ya lazima ya afya, wakati wale wanaopata shilingi milioni moja walichangia shilingi 1,700 pekee, ambayo ni sawa na asilimia 0.0017 ya mshahara wao," anaongezea.

Mfumo unaosubiriwa unalenga kuhakikisha kuwa hospitali zinapata fedha na rasilimali za kutosha ili ziweze kutoa huduma bila za afya bure.

Takwimu za serikali zinaonesha kuwa takribani watu milioni tatu tu wanapokea mishahara yao kila mwisho wa mwezi.

" Tuna watu ambao hawapati mishahara lakini wana aina tofauti ya mapato yatakayowawezesha kufurahia hii, halafu tutapima kuwa anatarajiwa kutozwa kiwango kipi cha bima ya afya ya jamii," alisema.

Wale ambao hawana kipato cha aina yoyote kwa sababu za maradhi au umri, serikali itaweka mpango wa kuwasaidia.

" NHIF haikuwahudumia watu kwa asilimia 100 , mfumo huu mpya hautochagua wala kubagua maradhi anasema Nakhumicha.