Kenya yafanya juhudi ya biashara ya kaboni

Kenya yafanya juhudi ya biashara ya kaboni

Rais William Ruto amevumbua pikipiki zisizototumia mafuta
Rais Ruto amevumbua pikipiki za kutumia umeme/ Picha ya Ikulu ya Kenya 

Serikali ya Kenya inasema imejitolea kuimarisha hatua ya kukumbana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kupitisha mifumo ya uchukuzi ya hewa ya chini ya kaboni.

Rais William Ruto alisema serikali itatumia teknolojia bunifu, safi na endelevu ya kawi.

Pikipiki za kutumia umeme zinalenga kupunguza gesi chafu hewani/ Picha kutoka Ikulu Kenya 

Rais Ruto, Ijumaa aliidhinisha Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Tabia nchi ambao ulichapishwa Julai.

Sheria hiyo inalenga ya kudhibiti masoko ya kaboni.

Ruto amesema pikipiki hizi za kutumia umeme zinaambatanza na malengo ya sheria hii.

Lengo sio tu kupunguza uzalishaji wa gesi chafu lakini pia kutoa usafiri wa bei nafuu na kuchochea ukuaji wa sekta ya magari ya umeme.

Kenya inapanga kuanza uchukuzi wa kaboni/ Picha kutoka Ikulu ya Kenya 

Magari ya magurudumu mawili na matatu yanajumuisha sehemu kubwa zaidi ya uhudumu wa usafiri wa kitaifa na hutumiwa zaidi na wananchi wengi.

"Kupitishwa kwa mifumo ya kutumia umeme kunaipa serikali uwezo wa kukumbana na changamoto za uchafuzi wa mazingira," alisema.

Rais Ruto, Ijumaa aliidhinisha Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Tabia nchi ambao ulichapishwa Julai/ Picha kutoka Ikulu ya Kenya 

Rais Ruto amewahakikishia hasa waendeshaji bodaboda kwamba uhamaji wa kielektroniki utaongeza mapato yao kwa kiasi kikubwa.

TRT Afrika