Maandamano yaliyoongozwa na upinzani yamefanyika mara kadhaa kupinga sheria ya fedha 2023/ Picha: AFP

Mahakama ya rufaa nchini Kenya imeondoa vikwazo vya sheria ya fedha 2023 ambayo ilikuwa imesimamishwa.

Sheria ya fedha 2023 ilipitishwa bungeni mwezi Juni lakini haikuweza kutimizwa kuanzia Julai kwasababu mahakama ilisimamiha kutimizwa kwake.

Kesi ya kupinga sheria ya fedha iliwasilishwa kotini kwa mara ya kwanza na seneta wa upinzani akitaka alkilalamika kuwa baadhi ya sehemu za sheria hiyo zinafaa kukomeshwa kwani ziko kinyume cha katiba.

Sheria hiyo ilisababisha maandamano makubwa ya upinzani mwezi huu huku wakidai kuwa itawaongezea gharama ya maisha.

Chini ya sheria hiyo mpya, ushuru wa ongezeko la thamani kwenye mafuta utaongezeka maradufu hadi 16% .

Wafanyakazi pia watakabiliwa na ushuru wa nyumba wa 1.5% ambao utalingana na waajiri wao.

"Maslahi ya umma yanaegemea upande wa kuweka kando maagizo ya kihafidhina na jaji wa mahakama," majaji wa rufaa walisema katika uamuzi wao wa Ijumaa.

Serikali ya Rais William Ruto inasema ongezeko ya ushuru ni muhimu ili kuongeza mapato ya ndani ya nchi na kuweza kulipa deni za nchi,

Katika kupinga sheria hiyo, muungano wa upinzani umefanya maandamano matano mwezi huu, ambayo baadhi yalisababisha makabiliano makali na polisi,

Zaidi ya watu ishirini waliripotiwa waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

TRT Afrika