Zaidi ya Madaktari 4,000 kutoka hospitali za umma wanashiriki katika mgomo./ Picha: Reuters

Mahakama ya nchini Kenya imewataka madaktari na serikali kufikia makubaliano ya kusitisha mgomo, ndani ya saa 48.

Madaktari kutoka hospitali za umma waliitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia katikati ya mwezi Machi wakishinikiza malipo zaidi na uboreshwaji wa mazingira ya kazi na hivyo kuathiri huduma za afya nchini humo.

Chanzo cha mzozo huo ni hatua ya serikali kupunguza mishahara ya wahudumu wa afya wanaofanya kazi kwa karibu asilimia 30 ya madaktari, kulingana na Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya.

Siku ya Jumatano, hakimu wa mahakama ya kuu, kitengo cha kazi Byram Ongaya alisema muungano wa kitaifa wa madaktari na serikali lazima waitishe mkutano mara moja "bila masharti" na kurudi kazini siku ya Ijumaa."

'Nia njema'

Mapema mwezi huu, madaktari hao walikataa ofa ya serikali iliyosema itakidhi baadhi ya matakwa ya matabibu, ikiwa ni pamoja na kuajiri wafanyakazi wa ndani kwa kandarasi za kudumu na kulipa malimbikizo yanayodaiwa chini ya makubaliano ya 2017.

Serikali imefutilia mbali makubaliano yoyote zaidi na makataa ya wiki mbili yaliyowekwa na mahakama ya kazi kumaliza mkwamo uliokwisha bila makubaliano siku ya Jumatano.

Ongaya aliamua kwamba pande zote lazima "zijadili kwa nia njema kabisa kuelekea maafikiano na kwa manufaa ya kurejesha huduma za afya kikamilifu."

Pia aliagiza kuwa muungano wa madaktari uhakikishe kuna idadi maalum ya madaktari katika hospitali zote kushughulikia dharura huku mazungumzo yakiendelea.

Kuongezeka kwa vifo

Gazeti la Daily Nation, kutoka nchini Kenya, siku ya jumatano liliripoti kuwa mvutano huo umesababisha vifo vingi, huku hakuna wataalam katika baadhi ya hospitali zinazotoa matibabu ya saratani.

Mamia ya wagonjwa sasa wameweka maisha yao rehani katika katika hospitali za kibinafsi na zahanati za vijijini, ilisema.

Migomo katika sekta ya afya ni kitu cha kawaida nchini Kenya.

Mnamo 2017, madaktari walifanya mgomo wa siku 100 nchini kote ambao uliacha hospitali za umma zimefungwa.

Kupuuza makubaliano

Wagonjwa wengi walipoteza Makumi ya wagonjwa walikufa kutokana na ukosefu wa matibabu wakati wa mgomo huo, ambao ulimalizika baada ya makubaliano ya mazungumzo ya pamoja kufikiwa.

Hata hivyo, madaktari wanaituhumu serikali kwa kukiuka baadhi ya makubaliano na kupelekea kuwepo kwa mgomo huo.

TRT Afrika