Rais wa Kenya William Ruto( wa pili kutoka upande wa kushoto) akiwa na viongoiz wa jamii ya Maa/ Picha kutoka X ya rais William Ruto 

Rais William Ruto amesema kuwa Kenya itafanya uwekezaji zaidi katika utalii wa tamaduni.

Utalii wa tamaduni unajumuisha ziara maalum katika tamaduni zingine na mahali pa kujifunza kuhusu watu wao, mtindo wao wa maisha, urithi na sanaa.

Jamii ya Maasai ni mojawapo ya vivutio vikubwa vya utalii nchini Kenya/ Picha kutoka X ya rais William Ruto 

Rais alihudhuria tamasha ya kitamaduni ya jamii ya Maa ambayo inajumlisha kabila la Wamaasai . Tamasha hii ilifanyika katika enoa la Sekenanie Gate, kaunti ya Narok.

"Mtalii wa leo anavutiwa na uzoefu halisi wa kitamaduni; kwa hivyo, utalii wa leo lazima ufikie kiwango cha juu,” alisema.

Shirika la UNESCO linatambua utamaduni wa Maasai kama urithi wa tamaduni muhimu duniani /Picha kutoka X ya rais William Ruto 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni( UNESCO) limebainisha sherehe ya wavulana kabla ya kwenda jandoni, kuwanyoa morani na sherehe ya kula nyama ambayo inaashiria kuingia katika utu uzima katika jamii ya Maasai, kama urithi wa tamaduni muhimu duniani.

Serikali ya Kenya itaanza kuzipa jamii ambapo kuna hifadhi za wanyama nusu ya mapato ili kuboresha maisha yao / Picha kutoka X ya rais William Ruto 

Rais Ruto amesema serikali itaanza kutoa asilimia 50 ya mapato kutoka kwa hifadhi za taifa kwa ajili ya kuboresha jamii ambapo hifadhi hizi zipo, kwa ajili ya 'kuboresha maisha ya jamii hizi.'

Mapambo ya kitamaduni ya Kimaasai/ Picha kutoka X ya rais William Ruto 

Mapambo ya kitamaduni ya Kimaasai ni mojawapo wa kivutio kikubwa kimataifa. Sekta hii tayari inaajiri maelefu ya watu kutoka jamii ya Wamaasai ambao wanaouza nchini na hata kwa masoko ya kimataifa.

Serikali inataka kuuza tamaduni zingine kwa ubora huu pia.

TRT Afrika