Serikali imetangaza kuwa itawaajiri wahudumu laki moja kukabiliana na changa moto ya kuwafikia watu vijijini Picha:  AP

Serikali ya Kenya itaajiri wahudumu wa afya wa jamii zaidi katika jitihada ya kupanua huduma za afya nchini.

Rais William Ruto amesema jumla ya wahudumu 103,000 wataajiriwa.

"Huduma ya afya ya kinga inaokoa maisha na rasilimali. Mtazamo huu kwa huduma kwa wananchi utaturuhusu kugundua maswala ya afya mapema na kudhibiti yale madogo katika ngazi ya jamii, jambo ambalo litapunguza foleni katika hospitali zetu na kuboresha utoaji wa huduma,” Rais Ruto alieleza.

"Tumekubaliana na serikali za kaunti kwamba tunafaa kusawazisha malipo ya waafisa hawa wa afya ya jamii na tunahitaji pia kusawazisha vifaa ambavyo vitapatikana ili watumie katika huduma ambayo watakuwa wakitoa katika kila kijiji," Ruto alisema.

Mhudumu wa afya ya jamii ni mtu ambaye amefunzwa kutoa huduma muhimu zaidi -kama vile huduma ya dharura ambayo inaweza kuokoa maisha watu wakiwemo watoto.

Katika taswira ya vijijini wakaazi wengi wanapendelea kufanya kazi na wahudumu wa afya ya jamii kwani wengi ni wazaliwa wa pale kijijini na kuaminika na wakaazi.

Kwa wale wanaohusika na huduma kwa watoto wanaweza kusaidia kuepusha vifo vya watoto kutokana na maradhi ya mara mara kama vile kipindupindu, homa ya mapafu malaria.

Wao ni hatua ya kwanza ya mawasiliano kwa wengi wakati wa changamoto ya kiafya. Huwa wanaishi ndani ya jamii na hivyo wanajua na kuelewa watu na tamaduni.

TRT Afrika