Kenya, Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati kuungana katika mapambano dhidi ya ugaidi

Kenya, Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati kuungana katika mapambano dhidi ya ugaidi

Marais wa nchi hizi tatu wamekutana nchini Kongo
Kenya, Jamhur ya Afrika ya kati na Congo zakubaliana kushirikiana katika kuinua usalama/ Picha: Ikulu Kenya

Marais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Denis Sassou N’Guesso wa Jamhuri ya Kongo na William Ruto wa Kenyaya wamekutana Jumapili huko Oyo, Jamhuri ya Kongo.

Nchi hizi zimeamua zitaungana katika mapambano dhidi ya ugaidi na ukosefu wa usalama barani.

"Nchi zetu zinahitaji kufanya kazi pamoja ili kutafuta suluhu zinazofaa kwa matatizo ya pamoja yanayokabili amani na usalama wa kimataifa na kikanda," Rais William Ruto alisema katika mkutano wao.

Nchi hizo tatu zilikubali kugawana habari za ujasusi na kuchukua misimamo ya pamoja kwenye majukwaa ya kimataifa ili kukuza ajenda ya amani ya Afrika.

Zilikubali zitafanya kazi kwa karibu katika kupambana na itikadi kali za kivita ili kufikia amani, usalama na utulivu.

Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na changamoto ya usalama kwa muda mrefu .

Mwaka 2020 makundi sita yenye silaha, yakiwemo ya zamani ya Seleka na anti-balaka, yaliungana na kuunda Chama cha Patriots for Change (CPC), muungano ulioungana kupinga serikali.

Juni 2023, Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba makundi mawili yenye silaha na makundi matatu ya wanamgambo kutoka eneo lililokuwa likishikiliwa na waasi kwa muda mrefu yalisambaratishwa.

Hata hivyo, changamoto za upokonyaji silaha na kuunganishwa tena zimesalia.

TRT Afrika