Umati wa watu wakiwa mbele ya kituo cha hija cha Namugongo nchini Uganda./Picha: Wengine

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mkewe Janet ni kati ya maelfu ya mahujaji waliofurika katika kituo cha Namugongo wakiadhimisha siku ya Mashujaa wa Uganda.

Watakatifu Mashahidi wa Uganda. Watakatifu hao waliuwawa kuanzia mwaka 1885 January 31 mpaka mwaka 1887 .

Mauaji yalifanywa katika viunga vya Kampala kulikofuatiwa na kuchomwa moto kwa Charles Karoli Lwanga na wenzake wengine huko Namugongo Uganda.

Baadhi ya mahujaji waliofurika katika eneo la Namugongo kaudhimisha siku ya Mashahidi wa Uganda./Picha:TRT Afrika

Mauaji yaliendelea tena Oktoba 18, 1918 walipouwawa Daudi Okello na Jildo Irwa, huko Paimol.

Mtakatifu Charles Lwanga na wenzake 22, walitangazwa wenye heri na Papa Benedict wa 15, Juni 6, 1920.

Kanisa Katoliki duniani likaamua kutenga siku maalumu ya kuwakumbuka Mashahidi wa Uganda, kila ifikapo Juni 3. Ilikuwa ni ishara ya kuwakumbuka Wakatoliki 22 na Waanglikana 23, walikubali kuifia dini yao kutokana na mateso waliyoyapata kutoka kwa Kabaka Mwanga, aliyekuwa mtawala wa iliyokuwa Buganda ambayo kwa sasa inafahamika kama Uganda, kati ya mwaka 1885 na 1887.

Mauaji yalifanywa katika viunga vya Kampala kulikofuatiwa na kuchomwa moto kwa Charles Karoli Lwanga na wenzake wengine huko Namugongo Uganda./Picha: Getty

Tukio hilo, lenye kuvutia watu wengi duniani, hukusanya maelfu wa mahujaji kutoka Uganda na mataifa mengine ya Afrika na Ulaya kufanya kumbukumbu ya wakristo 45, wakatoliki 22 na waanglikana 23, waliouwawa kwa chuki ya imani yao katika mwisho wa karne ya 19 na Kabaka Mwanga wa pili, aliyekuwa mtawala wa Buganda kwa wakati huo.

Waaumini hao hutembelea eneo hilo wakiwa na nia zao za maisha, wakiamini kuwa watapata baraka na heri maishani kwa kupitia maombezi ya watakatifu mashahidi wa Uganda.

Mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Maria Nyerere akiwasili katika Ikulu ya Uganda tayari kwa maadhimisho hayo./Picha: Wengine

Mjane wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere amekuwa akihudhuria kumbukumbu hiyo kwa miaka 17 sasa.

Mama Nyerere aliambatana na mumewe Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye hija hizo, kabla ya kifo chake mwaka 1999.

Pia, hija hiyo imekuwa ikihusishwa na mchakato Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu, kulingana na taratibu za Kanisa Katoliki duniani.

Mama Maria Nyerere akisalimiana na baadhi ya mahujaji waliohudhuria hija hiyo./Picha:TRT Afrika

Kila baada ya hija, waamini hurejea makwao na kumbukumbu muhimu kama vile maji ya baraka, vitabu na ishara nyingine kutoka Namugongo.

Rozari Takatifu na kumbukumbu muhimu wakati wa hija ya Namugongo./Picha: TRT Afrika.

Historia ya Mauaji

Uwepo wa Kanisa Katoliki barani Afrika pia ulichagizwa na uwepo wa Wamishioanari wa White Fathers, walioeneza imani hiyo, mwanzoni mwa karne ya 19.

Wakati huo Kabaka Mutesa wa Kwanza, ambaye alikuwa kiongozi wa Buganda aliruhusu uwepo wa Wamishionari hao ili kueneza dini ya Kikristu.

Uwepo wa Kanisa Katoliki barani Afrika pia ulichagizwa na uwepo wa Wamishioanari wa White Fathers, walioeneza imani hiyo, mwanzoni mwa karne ya 19./Picha: TRT Afrika.

Hata hivyo, hali ilibadilika wakati wa utawala wa Kabaka Mwanga, ambaye alimuua Askofu wa Kanisa la Kianglikana kwa wakati huo, James Hannington na wenzake, mnamo Oktoba 1885.

Joseph Mukasa, aliyekuwa moja ya watumishi watiifu wa Kabaka Mwanga hakufurahishwa na hatua hiyo, hata hivyo ilipofika tarehe 15 ya mwezi Novemba mwaka huo, Mukasa aliuwawa kwa kuchinjwa na Kabaka Mwanga mwenyewe.

TRT Afrika