Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete  | Picha: Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Tanzania

Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda ambapo alialikwa kama mgeni rasmi.

Mkutano huo uliojadili umuhimu na nafasi ya viongozi waliopo madarakani kuandaa viongozi wanaochipukia ulihudhuriwa na zaidi ya marais na viongozi wa sasa na waliowahi kuwa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchini Uganda zaidi ya 1,000.

Mkutano wa Jumuiya ya Afrika | Picha: Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Tanzania

Makamu wa Rais wa Uganda, Bi. Jessica Allupo na Waziri Mkuu Mstaafu wa nchi hiyo Ruhakana Rugunda pia walishiriki katika mkutano huo uliofanyikia katika Chuo Kikuu maarufu cha Makerere, Kampala nchini Uganda.

Pamoja na mambo mengine, washiriki wa mkutano huo, ambao wengi ni vijana, walijadili kwa kina na uwazi fursa, changamoto na matamanio yao kama vijana ambao tayari wameonesha uwezo wa kuongoza na namna serikali na jamii ya Uganda inavyoweza kuwatumia katika nafasi mbalimbali za kiongozi serikalini, kwenye mashirika mbalimbali na kwenye jamii kwa ujumla.

Mkutano wa Vijana | Picha: Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Tanzania

Aidha, suala la kufanya siasa za vyama ndani ya vyuo vikuu lilijadiliwa kwa kirefu ambapo washiriki walitofautiana maoni ambapo wapo walioona kuwa ushiriki kwenye siasa za vyama kwa wanafunzi waliopo vyuoni ni jambo la msingi katika kutetea maslahi ya wanafunzi na kuwaandaa wanafunzi kuwa viongozi na wanasiasa wazuri wa siku za usoni, huku wengine wakieleza mtizamo wao kuwa mwanafunzi makini anaweza kuwa kiongozi katika nafasi mbalimbali kwenye jamii bioa ya kufungamana na vyana vya siasa.

Waliounga mkono hoja hii walieleza kuwa, siasa vya vyama zinaweza kufungamanisha na kufunga mawazo mazuri ya kimaendeleo aliyonayo mwanafunzi kwa ajenda za kiasiasa za chama cha siasa ambacho ni mwanachama na kumfanya kutoona maeneo mengine kwenye jamii ambayo anaweza kuonesha uwezo wake wa kiuongozi.

Vijana wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wawe chachu ya utengamano katika Jumuiya kwa hatua zilizobakia za Umoja wa Kifedha na Shirikisho la Kisiasa.

Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Kwa upande wake Rais Mstaafu Kikwete aliwapa uzoefu wake katika siasa za vyuo vikuu alipokuwa Rais Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1972 - 1973 na namna alivyojifunza kipindi hiko umuhimu wa viongozi vijana kuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati.

Akawaasa viongozi hao kujifunza kujenga hoja za nguvu ya kufanya mabadiliko katika mambo wanayoyataka na kujiepusha na kishawishi cha kulazimisha jambo ambalo wakati wake bado haujafika au kwa kukiuka taratibu ambazo zimewekwa kwa makubaliano ya pamoja.

Akaongeza kuwa kijana yoyote, si lazima awe kiongozi, ana uwezo wa kutumia vyema kipaji chake, uwezo wake wa kufikiri na nguvu alizonazo kupaza sauti itakayoleta mabadiliko katika jamii na taifa lake kwa ujumla.

Julius Nyerere Leadership Centre | Picha: Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Tanzania

Aidha, kwa nafasi yake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Kikwete alieleza kuvutiwa kwake na ubunifu wa mkutano huo kwa kuwatanisha viongozi wa sasa na wa zamani wa vyuo vikuu pamoja na viongozi wa serikali kwani unatoa fursa ya kujadili na kulinganisha hatua zilizofikiwa katika kushughulikia masuala mbalimbali ambayo serikali za wanafunzi zimekuwa zikiyafuatilia kwa nyakati tofauti.

Vile vile, alishauri kuwa itakua jambo la busara kwa mkutano huo sasa kuandaliwa katika ngazi ya vyuo vyote kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kuwa jukwaa jingine la vijana kijadili masuala ya jumuiya na kuwa chachu ya kuharakisha jitihada za utenganamano wa kikanda katika nchi za EAC.

Rais wa Awamu ya nne Tanzania, Mrisho Jakaya Kikwete

Ripoti hii imetayarishwa kwa kiasi kikubwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania.

TRT Afrika