Jeshi la Israeli limefanya mauaji ya kimbari kaskazini mwa Gaza, Idara ya Ulinzi ya Palestina imesema.
"Hali inazidi kuwa mbaya kwa binadamu mashambulizi yakiendelea huko Beit Hanoun, Beit Lahia na Jabalia kwa siku ya nne mfululizo, hali inayotatiza upatikanaji wa maji, chakula na madawa," ilisema idara hiyo.
"Ubabe huu umesababisha mauaji ya kimbari dhidi ya raia na kupelekea vifo na majeruhi wengi," taarifa hiyo iliongeza.
Kwa mujibu wa idara hiyo, miili ya waathirika wa mashambulizi hayo ilikuwa imetekelezwa mitaani huku waokoaji wakishindwa kuibeba kutokana na mashambulizi ya Israeli.
Taarifa hiyo pia, ilibainisha kuwa jeshi la Israeli limetishia kuwahamisha kwa nguvu zaidi ya wakazi 200,000 waishio maeneo karibu na Gaza kaskazini.
TRT Afrika