Kikundi cha Houthi cha Yemen kimesema kuwa kilitumia "silaha mpya" wakati wa kuilenga na kuizamisha meli ya mizigo ya MV Tutor katika Bahari Nyekundu.
Taarifa hiyo ilitolewa na kikosi cha jeshi cha kikundi hicho na kurushwa kwenye televisheni ya Al-Masirah kinachomilikiwa na Houthi.
Kulingana na taarifa hiyo, "silaha mbalimbali za kivita zilitumika kuilenga na kuzamisha meli ya Tutor".
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, "Tukio hilo lilitokea baada ya chombo hicho kinachomilikiwa na kampuni ya Ugiriki, kukaidi agizo la kutokuingia bandari ya Haifa."
Taarifa hiyo pia iliituhumu meli hiyo "kwa kuzima mfumo maalumu wa utambuzi wakati kinakatisha katika Bahari Nyekundu."
TRT Afrika