Kila siku mwandishi wa habari anauawa, lakini kutoka kwa taasisi ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikihubiri kuhusu uhuru wa vyombo vya habari tunachosikia ni ukimya tu," rais alisema. / Picha: AA

Israel inalenga sio tu wanawake na watoto huko Gaza lakini pia waandishi wa habari wanaojaribu kufanya kazi chini ya hali ngumu, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

Mashirika ya kimataifa yanawajibika kwa kutokuwa na uwezo wa dunia wa kuanzisha amani na usalama duniani na kutatua matatizo, Erdogan alisema katika hotuba yake kwa Mkutano wa TRT World Forum 2023 mjini Istanbul siku ya Ijumaa.

"Makundi ya vyombo vya habari duniani yanajaribu kuficha ukatili unaofanyika Gaza na kuhalalisha mauaji ya waandishi wa habari kwa kisingizio cha Hamas," aliongeza, akizungumzia mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7, ambayo yamechukua maisha ya 17,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

"Kila siku mwandishi wa habari anauawa, lakini kutoka kwa taasisi ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikihubiri kuhusu uhuru wa vyombo vya habari tunachosikia ni ukimya," alisema.

Akivipongeza vyombo vya habari vya Uturuki kwa kuripoti habari za Gaza kwa usahihi, na kuonyesha hali halisi ya ulimwengu huko chini ya mzingiro mbaya, alisema:

"Ningependa kuwapongeza TRT, Anadolu, na vyombo vyetu vyengine vya habari ambavyo vilifungua ukanda muhimu kutoka Gaza hadi dunia.”

Zaidi ya waandishi wa habari 70 wameuawa huko Gaza, alisema Erdogan, na kuongeza:

"Viko wapi vyombo vya habari maarufu duniani?"

Magharibi kumwaga mafuta kwenye moto'

"Magharibi ambayo humwaga mafuta kwenye moto, siyo ambayo hulipa bei kwa kila dakika inayopotea katika kufikia amani ya kudumu, lakini kwa bahati mbaya watu wasio na hatia," rais wa Uturuki alisema.

"Uturuki iko tayari kubeba jukumu la kuzuia umwagaji damu zaidi kutokea (huko Gaza)," Erdogan alisema, akimaanisha pendekezo lake la kupatanisha amani au kuwa mdhamini wa eneo hilo.

"Katika amani ya haki, hakuna wapotezaji," aliongezea.

Zaidi ya waandishi wa habari 75 wameuawa na 140 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7.

Takriban Wapalestina 17,177 wameuawa na wengine zaidi ya 46,000 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga na ardhini huko Gaza tangu Oktoba 7 kufuatia shambulio la kuvuka mpaka la Hamas.

Idadi ya vifo vya Israel kutokana na shambulio la Hamas imefikia 1,200, kulingana na takwimu rasmi.

TRT Afrika