Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mulago nchini Uganda amezua hofu kuhusu ongezeko la tatizo la figo nchini Uganda. 

Hospitali ya Rufaa ya Uganda, Mulago Referral, imekana tuhuma za kuiba kwa viungo vya wagonjwa kwa ajili ya kuviuza.

Rosemary Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa Mulago Referral akiwa mbele ya Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya nchi hiyo, amekana madai ya wizi wa viungo vya wagonjwa katika hospitali hiyo.

Amesema kuna vipimo kadhaa na uchunguzi wa mgonjwa na wafadhili unaohitaji kufanywa kabla ya kupandikizwa kiungo chochote.

Byanyima aliwaelezea kuwa kufuatia mafanikio ya upandikizaji wa figo uliofanyika Disemba 2023, na timu ya wataalamu wa matibabu kutoka Uganda na wenzao kutoka India na Serikali, wagonjwa zaidi na wafadhili wao wanaendelea na matibabu.

Dkt .Byanyima pia aliibua wasiwasi juu ya ongezeko la visa vya magonjwa ya figo nchini Uganda, akisema kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za kusafisha damu kumeifanya Hospitali ya Mulago kufungua huduma hizo mapema saa kumi alfajiri kila siku.

Maambukizi ya figo ni aina ya maambukizi ya mfumo wa mkojo. Maambukizi ya figo yanaweza kuanza kwenye mrija unaosafirisha mkojo kutoka kwa mwili au kwenye kibofu. Maambukizi yanaweza kutokea katika figo moja au zote mbili.

"Pia tuna kitengo cha kusafisha damu na idadi ya mahitaji ya dialysis inaongezeka na tunaendesha kama vikao 4, kwa hiyo timu yetu inapaswa kuanza saa kumi asubuhi ili wafanye vikao vitatu ili kuruhusu muda wa kuhudumia na kusafisha. mashine,” alisema Byanyima.

TRT Afrika