MONUSCO ilichukua hatamu tarehe 1 Julai 2010 kutoka kwa oparesheni ya awali ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa iliyoitwa MONUC / Picha: AFP

Mipango ya kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa Nchini DRC, MONUSCO kuondoka nchini DRC unaonekana kubadilika, huku Kenya ikituma majeshi yake kuungana na kikosi hicho.

MONUSCO ni kikosi chini ya Umoja wa Mataifa kilichopo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

MONUSCO ilichukua hatamu tarehe 1 Julai 2010 kutoka operesheni ya awali ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa iliyoitwa MONUC.

MONUSCO iliidhinishwa kutumia njia zote muhimu kutekeleza majukumu yake, pamoja na mambo mengine, yanayohusiana na ulinzi wa raia, wafanyakazi wa kibinadamu na watetezi wa haki za binadamu chini ya tishio la unyanyasaji wa kimwili na kusaidia Serikali ya DRC katika utekelezaji wake katika juhudi za kuleta utulivu na uimarishaji wa amani.

Serikali ya DRC ilionyesha kutofurahishwa na kikosi hiki na Septemba 2023 Rais Felix Tshisekedi wa DRC akaamrisha waondoke.

"Inasikitisha kwamba Kikosi cha kulinda amani kilichotumwa kwa miaka 25 ... kimeshindwa kukabiliana na uasi na migogoro ya silaha," Tshisekedi alisema.

"Hii ndiyo sababu ... niliiagiza serikali ya Jamhuri kuanza majadiliano na mamlaka ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuharakisha kujiondoa kwa MONUSCO ... kwa kuleta mwanzo wa uondoaji huu wa hatua kwa hatua kutoka Disemba 2024 hadi Disemba 2023," alisema.

Wanajeshi chini ya MONUSCO

Kwa sasa Kenya inakuwa nchi ya 11 kutuma wanajeshi wake kuwa katika kikosi cha MONUSCO.

Kabla ya Juni 2025, MONUSCO ilikuwa na wanajeshi 13,500 lakini idadi hiyo ikapungua kwa 2000 baada ya kuondoka kufikia Juni 2024.

Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa na wanajeshi wake wa kulinda amani nchini DRC tangu 1999 / Picha: Reuters

Orodha ya nchi kumi zinazochangia wanajeshi kwa wingi ( Februari 2024)

Nchi wanajeshi

Pakistan 1908

India 1817

Bangaladesh 1676

Nepal 1153

Afrika Kusini 1135

Indosnesia 1035

Morocco 928

Tanzania 855

Uruguay 772

Malawi 758

Kikosi cha MONUSCO pia kina vikosi vya polisi wanaotoka nchi kama Senegal, Misri, Jordan, Bangladesh India , Niger, Djibouti, Burkina Faso, Tunisia na Togo.

Kuondoka kwa MONUSCO DRC

MONUSCO ilitangaza kuondoa majeshi yake nchini DRC.

Hata hivyo UN ilitangaza kusitisha kuondoka kwa kikosi hicho Julai 2024 bila kuweka ratiba ya lini itaendelea/ Picha: Monusco

Awamu ya kwanza ya uondoaji huo, katika jimbo la Kivu Kusini, ilikamilika Juni 25, huku wanajeshi 2,000 wa wakiondoka Kivu Kusini na kufanya kikosi cha sasa cha MONUSCO chenye wanajeshi 13,500 kupunguka hadi 11,500.

Hata hivyo, UN baadaye ilitangaza kusitisha kuondoka kwa kikosi hicho Julai 2024 bila kuweka ratiba ya lini itaondoa majesho yake tena, UN ikidai kuwa hali ya utulivu haijarejea katika eneo la Kivu kaskazini.

Kikosi cha MONUSCO DRC pia kina vikosi vya polisi kutoka zaidi ya nchi 10  /Picha:  Reuters 

Katika eneo hili kuna mvutano mkubwa kati ya wanajeshi wa serikali ya DRC, na kikundi cha waasi cha M23 . DRC inalaumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuwasaidia M23 lakini Rwanda imekana tuhuma hiyo.

Na sasa ikiwa kundi la kwanza la kikosi cha nne cha Kikosi cha wanajeshi wa Kenya Quick Reaction Force (KENQRF 4) kimetumwa rasmi DRC kuungana na kikosi cha MONUSCO, inaashiria kuwa MONUSCO haina mpango wa kuondoka kabisa kama ilivyodhaniwa hapo awali.

TRT Afrika