Bunge la Uganda limegundua kuwa leseni ya kampuni ya barua ya Posta Uganda muda wake ulimaliza mwaka 2021, na kampuni ina limbikizo la ada ya zaidi ya $465,000 ambayo ni sawa na shilingi bilioni1.7Bn ambazo hazijalipwa tangu 2017.
Ufichuzi huo ulitolewa na Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) kwa Kamati ya Bunge inayochunguza matatizo ya kifedha ya Posta Uganda.
“Tumekaa kimya kuhusu ada za leseni, tunawakumbusha, lakini hatuchukui hatua kali kama vile kuwanyang’anya leseni kwa sababu tulijua, nyie wakubwa wetu wa kisiasa ndani ya Bunge hamtatuuliza kwa nini hamkuondoa leseni ya Posta kwani hii ni mali ya taifa," Thembo Nyombi, Mkurugenzi Mtendaji wa UCC amewaambia wabunge.
Posta Uganda ndiyo mtoa huduma za usambazaji wa barua kitaifa, inayofanya kazi kupitia Ofisi za Posta zaidi ya 300 zilizo na masanduku ya barua zaidi ya 70,000 katika miji na miji mikuu zaidi ya 30 kote nchini.
Ilianzishwa mwaka 1951, kama msingi wa mawasiliano nchini Uganda.
Kamati ya bunge iliarifiwa kwamba Posta Uganda inadaiwa kodi ya zaidi ya dola milioni 1.5 ( sawa na shilingi bilioni 5.5) na Kampuni ya Simu ya Uganda.
Nayo Kampuni hiyo ya simu pia inadaiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani ya zaidi ya dola 383,000 ( sawa na shilingi bilioni 1.4) na Mamlaka ya Mapato ya Uganda, URA na zaidi ya dola 328,000 ( sawa na shilingi bilioni 2) za ziada za malimbikizo ya kodi ya Kukodisha kwa URA.
Nyombi, alilitaka Bunge kuhakikisha kuwa Posta Uganda inapewa kipaumbele na ipewe dhamana ikiwa itaendelea kudumu.
"Wanahitaji mtu wa kuwainua, hawawezi kuifanya peke yao. Uhandisi upya tunaouzungumzia unaotakiwa na Ofisi ya Posta una rasilimali nyingi sana za kifedha ambazo hawawezi kuzipata, hivyo mtu wa tatu hana budi kuwasaidia kwa mfano kufafanua biashara zao, jambo ambalo lazima lifuatiliwe na mpango wa uwekezaji na kwamba. itafuatiwa na uwekezaji," alifafanua Nyombi.
"Pesa zinapaswa kuwekezwa kwa Posta Uganda ikiwa tunataka kuendelea nayo. Serikali inapaswa kufanya uamuzi na kama watakuja kwetu, tutaiambia Serikali kwamba ndiyo, tunahitaji Posta iwepo,” aliongezea Nyombi.
Tume ya UCC ilitetea kusita kwake kufunga shughuli za Posta Uganda licha ya kushindwa kulipa leseni yake, ikitaja umuhimu wa kimkakati wa kuwa na kampuni ya Posta ya kitaifa.
Imesema hii inatimiza wajibu wa kimataifa wa Uganda katika Mkataba wa Umoja wa Posta unaoitaka Uganda kudumisha huduma za Posta.
Kulingana na UCC, ikiwa Posta Uganda haitaweza kumaliza changamoto zake za ufilisi, Mdhibiti anaweza kulazimika kutoa pendekezo kwa Serikali kuteua kampuni binafsi kama mwendeshaji wa kitaifa kama ilivyofanyika nchini Algeria, Misri na Morocco kwa sababu chini ya Mkataba wa Umoja wa Posta wa Kimataifa, kila mtu aliyetia saini lazima awe na opareta wa posta.