Haiti na Kenya wameanza mazungumzo juu ya jukumu la kupambana na vurugu za makundi ya uhalifu

Haiti na Kenya wameanza mazungumzo juu ya jukumu la kupambana na vurugu za makundi ya uhalifu

Polisi wa Haiti wamekuwa wakipambana na makundi yenye nguvu ya uhalifu yanayokadiriwa sasa kudhibiti sehemu kubwa ya nchi
Kundi la genge la G9 lilifanya maandamano ya kupinga dhidi ya Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, wiki hii huko Port-au-Prince, Haiti. / Picha: Reuters

Haiti na Kenya zimeimarisha uhusiano wa kidiplomasia siku ya Jumatano, kulingana na taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa X iliyotolewa wa Ariel Henry, Waziri Mkuu wa nchi hio ya Karibiani.

Hatua hii inakuja wakati wa majadiliano ya kimataifa juu ya uwezekano wa Kenya kuongoza kikosi cha usalama cha kimataifa kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusaidia polisi kupambana na ongezeko la vita vya makundi ya uhalifu nchini Haiti.

Serikali ya Henry ilisaka msaada wa kimataifa kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba uliopita, lakini licha ya wito mara kwa mara kutoka kwa Umoja wa Mataifa, ombi hilo halikupata majibu hadi Kenya iliposema ilikuwa tayari kuongoza kikundi kama hicho mwezi wa Julai mwaka huu.

Kupambana na makundi ya uhalifu

Kwa rasilimali chache, polisi wa Haiti wamekuwa wakipambana na makundi yenye nguvu ya uhalifu yanayokadiriwa sasa kudhibiti sehemu kubwa ya nchi.

Rais wa Kenya, William Ruto, na Henry walitia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano katika ubalozi wa Kenya huko New York, Marekani.

"Kama taifa linaloongoza katika jukumu la usalama la Umoja wa Mataifa nchini Haiti, tumejitolea kutuma timu maalum," Ruto alisema katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Timu hiyo itachunguza hali na kuandaa mikakati ya kuhakikisha suluhisho la kudumu, aliongeza.

Reuters