Polisi nchini Afrika Kusini wameanzisha msako wa kuwatafuta wahalifu waliohusika na kumuibia Waziri wa Uchukuzi, Sindisiwe Chikunga na walinzi wake wawili kwenye barabara kuu ya N3 kati ya Vosloorus na Heidelberg.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Athlenda Mathe, amesema kuwa mali binafsi na bastola mbili za huduma ziliibwa.
"Tangu wakati huo, jitihada za kuwatafuta wahalifu zimeanza kufuatia tukio hilo lisilo na kifani ili kuwaleta wale waliohusika na shambulio hilo. SAPS imejitolea kutekeleza agizo lake la kumlinda mtumishi wa umma na jamii kwa ujumla. Ulinzi wa watu mashuhuri (VIP) ni moja ya maeneo muhimu ya kipaumbele kwa SAPS na imefanywa kwa ubora zaidi ya miaka. Tunajitahidi kuendelea kutumikia na kulinda huku tukizingatia vipengele vyote vya itifaki zetu za ulinzi wa VIP," Polisi imesema.
Waziri Cele aliumbia mkutano wa Polisi na Magereza wa Umoja wa Haki za Kiraia (Popcru) huko Durban kwamba waziri huyo alikuwa akisafiri kutoka KwaZulu-Natal akielekea Gauteng wakati tukio hilo lilipotokea.
"Tukio kubwa lilikaribia kutokea wakati walipomimina risasi kwenye gari la Waziri Sindi Chikunga na wakaamuru kila mtu ndani ya gari, pamoja na Waziri Chikunga, alale chali, karibu tumpoteze waziri ambaye angepigwa risasi na kuuawa," ameongeza Cele.