Nchini DRC, likizo hii daima imekuwa ikisherehekewa kifamilia ambapo mchango wa upishi umekuwa muhimu sana. Mwaka huu katika eneo la mashariki mwa Kongo, Waislamu watatumia likizo hii chini ya matataizo ya kiuchumi kufuatia kupanda kwa kiwango cha dola nchini humo.
Waislamu siku zote wamekuwa wakitayarisha wali na nyama kwa ajili ya kuwagawia watu masikini ili wajisikie sawa na matajiri.
Watoto wa Kiislamu wanasubiri zawadi na nguo mpya kutoka kwa wazazi wao, lakini mwaka huu hali inaweza kuwa ngumu kidogo.
“Sasa sijapata pesa ya kuwanunulia watoto wangu chakula, inabidi niwaandalie vitu maalum ili waweze kuhisi hali ya sherehe,” alisema Asha Hassan, mwanamke wa Kiislamu kutoka Beni, DRC, aliyewasiliana na TRT Afrika.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina takriban wanawake Waislamu milioni tano katika wakazi wapatao milioni 90. Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini humo baada ya Ukristo.
“Nisipokuwa na uwezo tutanunua mbuzi tutakae gawana na familia nyingine sita,” aliongeza Bi Hassan.
Siku ya Eid Waislamu wanapata kifungua kinywa kisha asubuhi wanakwenda msikitini kuswali, baada ya hapo wanawake wanakwenda sokoni kununua mchele na nyama, ambayo huandaliwa kwa pamoja kutengeneza mchanganyiko uitwao “Pilau” ili kushiriki na familia na majirani.
Swala ya Eid inafanyika kwa saa moja katika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu mbele ya Waislamu mia moja.
Baada ya kumaliza kula, Waislamu wanakutana jioni kwenye ufukwe wa Ziwa Tanganyika, wote wakiwa wamevaa nguo mpya.
Nchini Senegal
Waislamu waliovalia kanzu nyeupe husali pamoja asubuhi katika msikiti mkubwa wa Dakar kabla ya wanawake hao kwenda sokoni. Waislamu wengi wa Senegal wanapendelea kula kuku na wali inayojulikana kama "Poulet". Takriban 96% ya wakazi milioni 8 wa nchi hiyo ni Waislamu.
Nchini Tunisia
Waumini wa Kiislamu huimba sifa kwa Mwenyezi Mungu, ambazo huenea katika eneo lote.
Waumini waliojitolea kulipa Zakat al-Fitr, wamevaa nguo nzuri kuashiria tabia ya kipekee ya siku hii, ambayo hushiriki wakati wa kutafakari kwa pamoja, kubadilishana mawazo, kutakiana heri na kutoa zawadi kwa watoto.
Eid Al-Fitr ni likizo bora ya familia. Watunisia hutembeleana nyumba kwa nyumba wakati wa siku tatu za tamasha hilo, wakiwa wamebeba masanduku yaliyojaa keki.
Wanaanza na babu na bibi, kisha wajomba na shangazi, binamu ... Wakikusanyika karibu na meza moja iliyojaa pipi za kitamaduni na keki zilizotayarishwa haswa kwa hafla hiyo, na mara nyingi hushirikiwa na jirani.