Wizara ya Mazingira na serikali ya mkoa wamekubali kutoa fidia ya Batwa ya eneo lililoorodheshwa na UNESCO la Kahuzi-Biega iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na ardhi ya kilimo, zahanati na shule. Picha: Reuters

"Kwa sasa tunachunguza mzozo wa ardhi kati ya jamii ya kiasili ya Batwa na mashirika ya kuhifadhi mazingira, na ripoti zitachapishwa," Jérémie Zirumana, Waziri wa mkoa wa Kivu Kusini, aliiambia TRT Afrika.

Mnamo mwaka wa 2019, mamlaka ya Kongo, haswa Wizara ya Mazingira na serikali ya mkoa, ilikubali kuwalipa kabila la Batwa kutoka mkoa wa Kahuzi-Biega, fidia ya uhifadhi wa turathi ya ulimwengu ya UNESCO, fidia iliyosubiriwa kwa muda mrefu, ikijumuisha shamba, zahanati na shule.

"Kwa sasa, ni taasisi ya uhifadhi ya maliasili ya Congo (ICCN) ambayo inasimamia mbuga ya Kahuzi-Biege, urithi wetu", anasema Waziri Zirumana.

Kufuatia ahadi ambazo hazijatekelezwa na serikali ya Kongo, Wabata, watu wanaoishi kwa kuwinda na kukusanya, wanatishia kurudi katika hifadhi ya masokwe ya Kongo, ambako waliishi kabla ya Mbuga ya Kitaifa ya Kahuzi-Biega kuanzishwa mwaka 1970.

Jamii ya Batwa wamesubiri muda mrefu bila kupata fidia walioahidiwa na aserikali baada ya kuondolewa ardhi yao asili ya msitu  Picha : Reuters

Gavana wa Kivu Kusini, Theo Ngwabidje Kasi, alikuwa amesema kuwa juhudi zinaendelea ili kuzuia kurejea kwa mbuga hiyo. Pia alisema mamlaka za mitaa hazikuwa na fedha zinazohitajika kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi ya tatizo hilo.

Katika mahojiano na TRT Afrika, Jean-Marie Kasula, rais wa jamii ya bilikimo katika kijiji cha Muyange, anasema ameshtushwa na serikali kuwa bado haijatekeleza ahadi hizi za 2019.

"Nina wasiwasi sana kuona watu wetu wakifa kwa njaa na magonjwa bila kupata riziki zao za jadi au njia mbadala ambazo tuliahidiwa," anaongeza Bw Kasula.

TRT Afrika ilijaribu kuwasiliana na Taasisi ya Uhifadhi ya ICCN kwa taarifa zaidi kuhusu mgogoro huo, lakini bila mafanikio.

Mojawapo ya makundi ya mwisho yaliyosalia ya Sokwe wa Mashariki (graueri), ambayo sasa yamesalia sokwe 250 pekee nchini DRC Picha : Reuters

Bw. Kasula alikashifu ahadi zisizotekelezwa za mamlaka ambazo, alidai kuwa zilikuwa zikipendelea sokwe adimu na kuwaharibia haki zao (Batwa).

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mwaka 2009, zaidi ya 90% ya watu wa kiasili (87,000) wa Batwa wamepoteza haki ya kumiliki ardhi yao asili, ambayo limegeuzwa kuwa eneo la uhifadhi.

Mbuga ya Kitaifa ya Kahuzi Biega ni eneo kubwa la msitu wa mvua wa kitropiki unaotawaliwa na volkano mbili za kuvutia zilizotoweka, Kahuzi na Biega, na ni nyumbani kwa wanyama matajiri wa aina mbalimbali.

Mojawapo ya makundi ya mwisho yaliyosalia ya Sokwe wa Mashariki (graueri), ambayo sasa yamesalia sokwe 250 pekee, wanaishi kwenye mwinuko wa kati ya 2,100 na 2,400 m.

Mbuga ya Kitaifa ya Kahuzi Biega ni eneo kubwa , na ni nyumbani kwa wanyama matajiri wa aina mbalimbali.  Picha : Reuters 

Inakadiriwa kuwa Wabata asilia 10,000 wanaishi karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Kahuzi-Biega (KBNP) katika vijiji vya muda, wakijitahidi kuishi kwa kuwinda na kukusanya mimea ya dawa msituni.

Malalamiko yao yanasikika katika msitu wa mvua wa Bonde la Kongo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

TRT Afrika