Serikali ya DRC imeanza uchunguzi kuhusiana na uvamizi na uharibifu wa jengo la makumbusho ya shujaa wa nchi hiyo Patrice Lumumba, lililotokea siku ya Jumatatu usiku.
Inaaminika kuwa, jengo hilo linahifadhi jino la kiongozi huyo wa zamani wa nchi hiyo, wizara ya utamaduni imesema siku ya Jumanne.
Lumumba alichaguliwa kama Waziri Mkuu wa nchi hiyo baada ya nchi hiyo kujitwalia uhuru wake kutoka kwa Wabelgiji mwaka 1960. Aliuwawa mwaka 1961 kufuatia kupinduliwa kwa serikali yake iliyodumu kwa miezi mitatu.
Inaaminika kuwa, jina hilo lilitolewa kutoka kwenye mwili wa Lumumba na askari wa Kibelgiji, ambaye alidai kuwa aliiuunguza mwili wa shujaa huyo.
Familia ya Lumumba ilikabidhiwa jino hilo mnamo mwaka 2022.
TRT Afrika