Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam Albert-John Chalamila amethibitisha kuwa shughuli ya uokoaji bado inaendelea katika jengo lililoporomoka mtaa wa Kariakoo jijini Daresalaam.
Chalamila amesisitiza kuwa kunao watu waliohai wamenaswa kwenye vifuzi na wanafanyakila juhudi kuwafikia salama.
''Kuna watu asubuhi hii tunawasiliana nao ambao wako upande wa basement. ambao tumeshawafikia kwa kuwapatia Oxygen, maji na glucose, na tunaendelea kuwatuliza wawe wastahamilivu tutawafikia,'' amesema Chalamila katika kuhutubia wanahabari eneo la mkasa.
Taarifa kufikia Jumapili asubuhi zinasema kuwa waliofariki wamefikia watu watano huku wengoine 45 wameopolewa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
Hata hivyo taarifa kutoka hospitali ya Muhimbili iliyoko jijini Daresalaam inasema kuwa walipokea wajeruhi 40 japo 33 kati yao wametibiwa nakuruhusiwa kwenda nyumbani. 7 ndio bado wamelazwa wakiendelea kupokea matibabu.
Miongoni mwa wanaosaidia katika uokozi ni Jeshi la polisi, Maafisa wa huduma ya dharura wengine. Mkuu wa Mkoa pia amesema ofisi ya waziri mkuu inasimamia na kuongoza oparesheni ya uokoaji.
Mkasa huo wa jengo hapo Kariakoo sio itu cha ajabu kwani kumekuwa na visa mara kwa mara huku hofu ikilelekezwa kwa uvunjaji wa kanuni za usalama wakati wa ujenzi na hivyo majengo mengi yanahofiwa kuwa hatarini.
Bado haijabainika kilichosababisha jengo hili kuporomoka siku ya Jumamosi lakin uchunguzi umeanzishwa.